Meneja wa England Roy Hodgson amempa tano mlinda mlando Joe Hart na kwamba ndiye mlinda mlango wake namba moja.
Mlinda mlango huyo wa Manchester City alikosolewa vikali kwa kiwango chake alichokionyesha wakati wa mchezo wa jumatano wa kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa mabingwa wa Ulaya Bayern Munich.
Hart mwenye umri wa miaka 26, amejiunga katika kikosi cha England kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Montenegro na Poland huku Wayne Rooney naye akirejea akiwa yuko fiti.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United alikosekana katika kikosi cha timu yake katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsks baada ya kumatwa na maumivu akiwa mazoezini.
Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge pia amerejea kutoka katika maumivu na atakuwepo katika kikosi cha wachezaji 23 wa ENGLAND.
Hart ambaye amekwisha kuitumikia England jumla ya michezo 35 ya kimataifa na kutunza clean
sheets katika michezo miwili ya mwisho ya England ya kufuzu kombe la dunia hakuwa katika kiwango chake katika mchezo dhidi ya Munich akifanya makosa mara mbili kushindwa kuzuia michomo ya Franck
Ribery na Arjen Robben.
No comments:
Post a Comment