Nyota huyo mzaliwa wa Brazil ambaye alianza kucheza soka nchini Hispania (Rojiblancos) mwaka 2007,ameamua kubadilisha uraia baada ya kupewa uraia wa nchi hiyo kufuatia baada ya kuwepo nchini hapo kwa miaka mitano ambayo imepelekea kuhamia la Roja baada ya kukosa kuiwakilisha Brazil maarufu kama Selecao.
Kocha Vicente Del Bosque hivi karibuni alikuwa akimuhimiza nyota huyo wa Atleti kubadili uraia na kwa mujibu wa shirikisho la soka la Hispania RFFF ni kwamba Costa ametamka kwa mdomo kukubali kuhusishwa katika kikosi cha mabingwa hao wa dunia.
Hata hivyo nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 hatakuwa halali kuchaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania katika michezo ijayo ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Belarus na Georgia kutokana na hali urasimu "bureaucracy".
Taarifa iliyonukuliwa hii leo imesomeka

"Diego Costa anataka kuichezea timu ya tauifa ya Hispania licha ya urasimu kumzuia katika muda huu.
"Mchezaji huyo wa Atletico Madrid Diego Costa hawezi kuchaguliwa kesho na meneja Vicente del Bosque kwa ajili ya michezo ijayo dhidi ya Belarus na Georgia kwani FIFA wamehitaji vielelezo zaidi vya maandishi ambavyo tayari wamesha vichukua licha ya kwamba mchezaji huyo amesha mueleza kocha wa Hispania kwa mdomo juu ya kutaka kwake kuichezea timu ya taifa ya Hispania hapo baadaye."

No comments:
Post a Comment