Bingwa wa Olimpiki na dunia na anayeshikilia rekodi
ya ulimwengu katika mbio za mita mia nane kwa wanaume mkenya David
Rudisha, amejiondoa kutoka kwa mashindano yajayo ya dunia
yatakayofanyika mjini Moscow Mwezi Ujao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya
habari, na naibu makamu wa rais wa shirikisho la mchezo wa riadha nchini
Kenya, David Okeyo, Rudisha hatalitetea taji lake mwaka huu kutokana na
jeraha.
Okeyo amesema baada ya kushauriana na
mwanariadha huyo pamoja na makocha wake, imebainika kuwa Rudisha bado
angali anauguza jeraha na haitakuwa vyema kwake kushiriki katika
mashindano hayo kwa kuwa inaweza kuhatarisha zaidi jeraha hilo.
''Nasikitika sana kuwa siwezi kuteteza taji
langu la mita mia nane mjini Moscow. Jeraha langu la mguu halijapona kwa
wakati ufaao ili kuniwezesha kushiriki katika fainali hizo za dunia.
Kwa hivyo nawatakia wanariadha wenzangu kila la heri katika mashindano
hayo ya dunia yatakayofanyika mjini Moscow.'' Amesema Rudisha.
No comments:
Post a Comment