Fabregas mawindo mapya ya bosi mpya wa United David Moyes.
Bosi
wa Manchester United David Moyes
ameonekana kukatishwa tamaa na kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas ambaye
amweleza meneja wake Tito Vilanova kuwa anataka kusalia katika kigogo
cha Katalunya.
United
ilithibitisha hapo jana kuwa imezindua nia yao ya kumnasa kiungo huyo
wa zamani wa Arsenal kwa ada iliyowekwa mezani ya pauni milioni £26.
maamuzi hayo yalikuja baada ya Thiago Alcantara kuamua kuungana tena na meneja wake wa zamani Pep
Guardiola katika klabu ya Bayern Munich badala ya mabingwa hao wa ligi kuu ya England Barclays Premier
League.
Habari za hivi karibuni zinaarifu kuwa bosi wa Barca Vilanova ameweka wazi kuwa na mazungumzo na Fabregas ambaye tayari ameweka wazi kuwa anataka kusalia Nou Camp.
Vilanova
amenukuliwa akisema
'Cesc amepokea ofa nyingine kutoka vilabu vingine. Nimezungumza naye ameniambia kuwa anataka kusalia. Ndoto yake ni kushinda mataji hapa.
'Tunafurahia kuwa naye Cesc. Nina uhakika kuwa amepokea ofa nyingi lakini amesema anafurahi kuwa hakuna nafasi kwake ya kuondoka.'
Kumekuwepo na taarifa nzuri zaidi kwa mashabiki wa Barcelona kwamba kiungo Sergio
Busquets amesaini mkataba wa nyongeza katika siku yake ya kuzaliwa mkataba ambao utamuweka Nou Camp mpaka June 2018.
Busquets ambaye amefikisha miaka 25 hii leo ,wakati ambapo anachukuliwa kama ni shujaa wa Barcelona akiwa katika kikosi cha kwanza katika jumla ya michezo 238.
Busquets ameongeza mkataba na kwa miaka mingine minne.
Wachezaji wa Barca wakiwa wameanza maandalizi ya msimu mpya.
Vilanova
No comments:
Post a Comment