Thiago Alcantara amethibitisha kwamba Pep
Guardiola (kulia pichani), ambaye ni bosi wake wa zamani wa Barcelona, ndiye aliyemfanya ajiunge na Munich kwa ada ya pauni milioni £22 usajili ambao umekamilika hii leo.
Nyota mpya wa Bayern Munich Thiago
Alcantara ametanabaisha kuwa Pep Guardiola ndiye aliyemshawishi kusaini kwa mabingwa soka barani Ulaya badala ya kuelekea kwa mabingwa wa soka nchini England Manchester United baada ya kukamilisha usajili wake ndani ya klabu hiyo uliogharimu kiasi cha pauni milioni £22.
Nyota huyo wa kimataifa wa kikosi cha Hispania cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 21 amesaini mkataba wa miaka minne mabingwa hao wa msimu uliopita wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, kikombe cha DFB-Pokal na Ligi ya mabingwa Ulaya na kusema isingekuwa rahisi kuacha na kusubiri kufanya kazi na kocha huyo mpya wa Bayern.
Amenukuliwa akiwa Munich akisema
'Nimecheza chini yake katika kikosi cha vijana cha Barcelona na namshukuru kwa kila kitu katika mafanikio yangu'
Thiago akikabidhiwa jezi namba 6 na mtendaji mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge
Wakikumbatiana baada ya kutambulishwa rasmi mjini Munich.
Thiago anaungana na Mario Gotze wakiwa sura mpya wakitarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi hicho ambacho kilitwaa kila taji waliloshindana msimu uliopita.
Thiago amesaini mkataba wa miaka minne na Bayern
No comments:
Post a Comment