Edinson Cavani ametajwa kujiunga naPSG baada ya kukamilisha uhamisho wa pauni milioni £55.
Cavani kwasasa ndiye mchezaji ghali wa wanne katika kipindi chote.
Paris St Germain hatimaye imekamilisha usajili wa mshambuliaji Napoli mwenye thamani kubwa Edinson Cavani kwa ada ya pauni milioni £55 kwa mkataba wa miaka mitano.
Cavani
alikuwa akihusishwa na vilabu vingibarani ulaya katika kipindi cha uhamisho cha kiangazi ikiwemo Manchester City, Chelsea na Real Madrid.
Amenukuliwa Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi akisema
'Kuwasili kwa Edinson Cavani
ni kielelezo kuwa uwezo wa klabu hii kuwavutia wachezaji wakubwa duniani'
Cavani amekuwa na makali tangu ajiunge na Napoli akitokea kwa wapinzani wakubwa wa Italia Palermo mwezi Julai 2010, ambapo amefunga jumla ya mabao 104 katika jumla ya michezo 138 aliyoichezea Napoli maarufu kama
Partenopei.
Alikuwa katika kiwango cha juu msimu uliopita akifunga jumla ya mabao 29 na kuisaidia Naples kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A.
Cavani akionekana pichani akiwa na mwenyekiti wa PSG Nasser Al-Khelaifi tajiri wa Qatar
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anakuwa ndiye mchezaji wa hivi karibuni kusajiliwa kwa pesa nyingi kutoka kwa Wafaransa hao ambao walikwisha kufanya hivyo huko nyuma kwa nyota wengine kama Zlatan Ibrahimovic, Marco Verratti,
Ezequiel Lavezzi, Lucas Moura, Javier Pastore na Thiago Silva miaka kadhaa iliyopita.
Cavani
anatazamiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji akiwa sambamba na Ibrahimovic, ambaye alitajwa kuwa mchezaji bora wa msimu uliopita katika ligi ya Ufaransa Ligue 1baada ya kufunga jumla ya mabao 30 msimu uliopita.
Bosi mpya wa PSG Laurent Blanc pia atakuwa akimtegemea Cavani na kiungo Lavezzi
kuonyesha kandanda safi na la kuvutia katiki kipindi chote cha utumishi wao Napoli
No comments:
Post a Comment