Wayne Rooney akasirishwa na kuchanganywa na hatma yake ndani ya klabu ya United.
Rooney anadhani hakuna cha kudhihirisha ubora wake ndani ya Old Trafford baada ya misimu tisa.
Inavyoonekana wazi sasa ni kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa England na Manchester United Wayne Rooney sasa anakaribia kuihama klabu yake ya Manchester United kabla ya kuanza kwa msimu mpya baada ya kuonyesha hasira zake waziwazi ndani ya klabu hiyo wakati huu ambapo klabu yake hiyo ikitafakari juu ya hatma yake ya baadaye.
Chelsea na Arsenal wote wako kwa njia kumnasa mshambuliaji huyo wa England ambaye ameripotiwa kuonyesha hasira na kuchanganyikiwa na jinsi anavyofanyiwa ndani ya klabu hiyo.
Maneno ya hivi karibu kutoka kwa mtendaji mkuu wa United Ed Woodward yanaeleza kuwa Rooney itabidi athibitishe ubora wake ndani ya kikosi katika wakati ambao Robin van Persie ni majeruhi.
Licha ya kwamba Van Persie aliongoza katika ufungaji msimu uliopita, Rooney anadhani si sawa kuwa katika nafasi ya kusubiri kuwa nje kutoka kwa mtu yoyote ndani ya Old Trafford.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni ni kwamba Rooney anadhani hana cha kuthibtisha ubora wake ndani ya kikosi cha United baada ya kuitumikia klabu hiyo misimu tisa akijibu kauli iliyoripotiwa kutolewa na Woodward katika vyombo vya habari.
Rooney
masaa 24 yaliyopita alisitisha ziara na klabu yake ya United ya maandanlizi ya msimu na kurejea nyumbani baada ya kuarifiwa kupatwa na maumivu jambo ambalo lililozua wasiwasi juu ya umara wa afya yake kwasasa.
Bosi wa Chelsea Jose Mourinho aliongea wiki iliyopita juu ya nia yake yake ya kumtaka Rooney,
akinukuliwa
'Ni mchezaji, nampenda sana lakini siwezi kuongea zaidi.
'Ana kasi, na ananyooka nina mpenda. Lakini ni mchezaji wa Manchester United.'
Van Persie anayemsubirisha Rooney benchi |
No comments:
Post a Comment