Jose Mourinho na Chelsea wajitosa rasmi kutaka saini ya Wayne Rooney
Mourinho akichati na mtendaji mkuu wa klabu yake ya Chelsea Ron Gourlay.
Jose Mourinho ameweka wazi kuwa Wayne Rooney
alikuwa ni chaguo pekee na mchezaji pekee ambaye Chelsea ilikuwa ikijaribu kumsajili msimu huu wa kiangazi.
Rooney
kwasasa yuko katika ya vilabu vya Chelsea na United licha ya United kukataa ofa ya mchezaji huyo.
Chelsea imethibitisha kuwa inataka kumnunua Rooney, ambaye ameingia katika mgomo na klabu yake ya United baada ya meneja wake David Moyes kuropoka jambo kwa waandishi wa habari huko Bangkok wiki iliyopita.
United pia imeonekana kukataa wazo la kupewa wachezaji wawili David Luiz au Juan Mata kama mpango wa kubadilisha na Rooney.
Akiongea akiwa Bangkok baada ya kushinda mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge kwa mara ya pili na Chelsea kama meneja baada ya kuichapa Singha All- Stars kwa bao 1-0, Mourinho bado ameonekana kutokukata tamaa juu ya wazo hilo.
No comments:
Post a Comment