Steven Gerrard |
Venue: Olympic Stadium
Nahodha wa
timu ya taifa ya England Steven Gerrard atakuwa hii leo akiingia uwanjani na
wasiwasi mkubwa wa kuondoshwa katika michuano hiyo kutokana na kumbukumbu ya
kutolewa kwa mara kwa mara Uingereza katika michuano mikubwa hasa inapofikia
katika hatua kama hii ya robi fainali.
Uingereza
usiku wa leo inaingia dimbani katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Euro
2012 dhidi ya Italia mjini Kiev.
Steven Gerrard akiwa na mkewe |
Gerrard atakuwa
akiwaongoza wenzake chini ya kocha Roy Hodgson wakiwa na kumbukumbu ya
kuondoshwa Euro 2004 na Ureno kwa njia ya penati mjini Lisbon na miaka mingine
miwili baadaye katika fainali ya kombe la dunia kule Gelsenkirchen.
Ananukuliwa Gerrard
akisema
"tangu
kuanza kuichezea England nimekuwa katika ndoto ya kufanya vizuri katika
michuano mikubwa na mpaka sasa haijatokea "
Gerrard akaongeza
"kuna
nafasi nyingine ya kufanya hivyo kwasababu maumivu ambayo nimekuwa nayo huko
nyuma na nadhani safari hii itakuwa tofauti. Nitafanya kila linalowezekana
kujaribu kufanya tofauti."
No comments:
Post a Comment