Andre Villa-Boas kocha mpya wa Tottenham Hospurs |
Meneja wa
zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas ameteuliwa kuwa meneja mpya wa Tottenham
Hotspur ikiwa ni wiki tatu baada ya kuondolewa kibaruani kwa mtangulizi wake Harry
Redknapp.
Villas-Boas
mwenye umri wa miaka 34 anarejea katika medani ya soka akiwa na mkataba wa miaka
mitatu katika kipindi kisicho zidi miezi minne tangu kuondoshwa Chelsea.
Kocha wa
zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Laurent Blanc, Roberto Martinez wa Wigan,
Fabio Capello na mshambuliaji wa zamani wa Spurs Jurgen Klinsmann walikuwa
wakihusishwa na kazi hiyo.
Maisha ya
Boas katika soka
1977: Born in Porto 17 October
1993: Works as a trainee under Sir Bobby Robson at Porto
1994: Achieves Uefa C coaching licence in Scotland
2002: Becomes part of Jose Mourinho's staff at Porto
2004: Follows Mourinho to Chelsea
2008: Moves with Mourinho to Inter Milan
2009: Appointed manager of Academica
2010: Named Porto boss
2011: Wins league, cup and Europa League in first season
2011: Appointed Chelsea manager
2012: Sacked by Chelsea after a 257-day reign at Stamford Bridge
Tottenham imetoa
taarifa hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa klabu hiyo wa Twitter.
Imenukuliwa taarifa
hiyo kupitia mtandao huo ikisomeka "klabu ina furaha kumtangaza Andre
Villas-Boas kama kocha mkuu,".
Maamuzi ya Tottenham
kumfukuza kazi Redknapp yalikuwa ni baada ya wiki kadhaa za mvutano kati ya
kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 na mwenyekiti wa klabu Daniel Levy.
No comments:
Post a Comment