KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, December 6, 2013

ROBO FAINALI CECAFA CHALLENGE CUP: MCHECHETO WA MSEBIA MICHO NI KWA SAMATA NA ULIMWENGU

Kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Uganda'Uganda Cranes' Mulitin ‘Micho’ Sredojevic anatazamia kukutana na kigingi cha timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro stars katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya michuano ya GOtv Cecafa Cup 2013 mjini Mombasa hapo kesho.
Kocha huyo msebia kikosi chake mpaka sasa bado hakijarusu goli na kuweka rekodi ya kushindamichezo yote mitatu lakini sasa kocha huyo anasema mpira wa kweli sasa ndio unaanza baada ya hatua ya makundi kukamilika.
Akinukuliwa Micho amesikika akisema
“Nkipongeza kikosi changu kwa kufikia hatua hii lakini mpira wa kweli unaanza sasa katika robo fainali.
“tunacheza na timu nzuri ambayo imepata nguvu mpya ya kisaikolojia baada ya wachezaji wake wawili kujiunga nayo wanaochezea TP Mazembe Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata”.
Mbwana na Ulimwengu walikosekana katika michezo miwili ya kwanza ya hatua ya makundi walipokuwa wakitoa huduma katika klabu yao katika michuano ya kombe la shirikisho na tayari wamengana na wenzao katika mchezo dhidi ya Burundi ambao Samatta alifunga goli pekee la Kili Stars.

Pamoja na kwamba Micho anategemea mchezo mgumu anaamini kuwa kikosi chake kinaweza kuitoa Kili stars mashindanoni.

“Nategemea mchezo mgumu lakini nategemea ushindi kama ambavyo watu wengi wanavyoipa nafasi timu yangu. Naiheshimu Tanzania lakini wakati huohuo nawaamini wachezaji wangu kufanya kile kinachotakiwa.”

Mshindi wa mchezo huo atakutana na ama wenyeji Kenya au Rwanda kwenye nusu fainali.

No comments:

Post a Comment