Bosi wa Manchester City Roberto
Mancini amekumbwa na hofu kubwa ya kuwakosa wachezaji wake ndugu wawili toka
familia moja Yaya na Kolo Toure ambao wanatarajiwa kuwemo katika kikosi cha
timu ya taifa ya Ivory Coast katika
fainali za mataifa nchini Afrika kusini .
Michuano hiyo imepangwa
kuanza januari 19 na kumalizika Februari 10 na hivyo huenda wakakosekan katika
michezo kadhaa ya klabu yao ya City.
Kama ilivyo kwa kiungo Yaya na
mlinzi Kolo, kiungo mwingine Adbul Razak huenda naye akaitwa katika kikosi
hicho cha Ivory Coast.
"ningependelea wasiende
katika michuano hiyo lakini ni ngumu, tutahitaji kuongea na meneja" amesema
Mancini.
"kama tutamkosa Yaya,
Kolo na Abdul, pamoja na kwamba hatumiki katika ,michezo mingi itatuwia vigumu
kupata mchezaji mchezaji wa kubadilisha endapo tutapa majeruhi."
Yaya ambaye ameitumikia Ivory
Coast michezo 67, anatajwa kuwa ni miongoni mwa viungo bora duniani na ni ngumu
kwa kocha wa Tembo Sabri Lamouchi kumuacha kiungo huyo katika kikosi chake kwa
ajili ya michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment