JESHI la Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kukamata baadhi ya vitu vilivyoporwa kufuatia ajali iliyosababisha kifo cha msanii wa
maigizo na muziki wa kizazi kipya nchini hapa, Hussein Ramadhani Mkiety
maarufu kama Sharo Milionea ambaye alikufa baada ya gari aliyokuwa
akisafiria kuacha njia na kupinduka.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa
Tanga, Constantine Massawe amesema kuwa vifaa hivyo vimepatikana kumetokana na jeshi la Polisi kufanya msako mkali kwa kushirikiana na
wananchi wa Kijiji cha Songa Maguzoni.
Kamanda Massawe amesema msakohu umefanikiwa kukamatwa kwa
vitu hivyo mbalimbali, zikiwemo nguo alizokuwa amevaa marehemu
Sharomilionea.
Massawe alivitaja miongoni
mwa vitu vilivyokamatwa ni Betri ya gari na Redio ya gari vilikuwa katika gari la marehemuj pamoja na tyrebegi
lililokuwa na nguo alizovuliwa marehemu siku ya ajali ambazo
inadhaniwa kuwa ndizo alizokuwa amezivaa, ikiwemo sambamba na mkanda,suruali na saa
ya mkononi.
Aidha alisema kwamba watuhumiwa walioiba vifaa hivyo
walimtumia mtu mmoja ambaye alikwenda kuvisalimisha kwa Mwenyekiti wa
Serikali ya Kijiji hicho cha songe, Abdi Zawadi ambapo wengine wanaotuhumiwa
kuhusika na wizi huo wakihama kaya zao wamekimbia.
Alisema
kuwa Polisi walifanikiwa kuikamata simu hiyo ya mkononi ya marehemu aina ya
Blackberry ambayo tayari ilikuwa katika mikono ya mnunuzi na
ilishaondolewa chipu kwa lengo la kuuzwa.
“Baada ya kuweka mtego wa kuinunua tumeikuta tayari imeshaondolewa chipu
sasa sijui ilikuwa na hela lakini vitu vingine vimesalimishwa kwa
Mwenyekiti wa Kijiji “,alisema Kamanda huyo.
Hata
hivyo alisema kuwa licha ya watuhumiwa wa wizi huo kufahamika lakini
wamekimbia makazi yao tangu kuanza kwa msako huo na kwamba Jeshi la
Polisi linaendelea kuwatafuta.
Marehemu
Sharo Milionea aliiaga dunia usiku wa kuamkia Novemba 27 mwaka huu
majira ya saa 2.00 usiku eneo la Songa-Maguzoni wilayani Muheza mkoani
Tanga katika barabara Kuu ya Segera kwenda Tanga baaada ya gari
alilokuwa akiendesha kuacha njia na kupinduka.
Sharo Milionea alizikwa Novemba 28 mwaka huu huko Kijijini kwao Lusanga wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment