Wenyeji wa
michuano ya kombe la chalenji Uganda Cranes wameendeleza wimbi la ushindi la
michuano hiyo baada ya hii leo kushomoza na ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi
ya Sudani kusini.
Ubao wa
mabao ulianza kusomeka kuanzia dakika ya 21 baada ya Brian Umony kuanzisha
karamu hiyo kabla ya kipindi cha pili kunako dakika ya 47 Robert Sentongo kuandika
bao la pili.
Bao la tatu
la Cranes liliwekwa kimiani na Hamis Diego Kiiza kunako dakika ya 79.
Ushindi huo
umewapa uongozi wa kundi A timu ya taifa ya Uganda wakikamilisha alama 9 na
magoli 6.
Michezo ya
makundi mengine itakamilishwa hapo kesho na michezo hiyo ikihamishiwa katika
viwanja vya KCCA huko Lugogo na Wankulukuku
No comments:
Post a Comment