Rais wa
shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesisitiza kuwa mshambuliaji wa Santos
ya Brazil Neymar anapaswa kuondoka
katika ardhi ya nyumbani ya Brazil la kuelekea kuecheza soka barani Ulaya
endapo anataka kushinda tuzo ya Ballon d'Or.
Mshambuliaji
huyo hakuorodheshwa katika orodha fupi ya majina ya wanao wania tuzo hiyo
lakini Blatter mwenye umri wa miaka 76 anasema mchezaji huyo anaweza kuwa na
nafasi ya kushinda lakini kwanza aondoke katika ardhi ya nyumbani.
"Neymar
yuko vizuri lakini ni vigumu kwa yoyoye asiyecheza soka Ulaya kuwemo katika
orodha hiyo ya mwisho"
Blatter
ametoa maneno hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Sao Paolo.
"kiwango
cha soka nchini Brazil ni cha juu, lakini soka barani Ulaya ndio kipimo cha
wachezaji".
Mshambuliaji
wa zamani wa kimataifa wa Brazil Ronaldo amekubaliana na maneno hayo ya
kiongozi wa FIFA, kukubali juu ya uwezo wa Neymar.
"Neymar yuko katika orodha ya wachezaji 23
walioteuliwa kwa ajili ya tuzo na hayo ni mafanikio, lakini nadhani kuwemo
katika orodha ya wachezaji wa mwisho anapaswa kucheza Ulaya au awe katika
kiwango cha juu katika timu ya taifa katika fainali za kombe la dunia 2014.
"Neymar
ni mchezaji mkubwa Brazil, lakini hajulikani Ulaya "
No comments:
Post a Comment