KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 1, 2012

Manchester City yaongoza kuwalipa mawakala wa wachezaji.



 Manchester City imetumia zaidi ya pauni milioni £10 kuwalipa mawakala wa wachezaji katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Mabingwa hao wa soka wa ligi kuu nchini England ‘Premier League’ wametumia jumla ya pauni milioni £10.5 ambazo ni zaidi ya pauni milini £2 walizotumia Liverpool ambao walitumia pauni milioni £8.6 kati ya kipindi cha Oktoba 2011 na Septemba 2012.

Hesabu za hivi karibuni za vipindi viwili vya uhamisho zinaonyesha kuwa nayo Queens Park Rangers nayo imetumia kiasi kikubwa katika kujaribu kuinusuru timu hiyo kusalia katika ‘Premier League’.

QPR, ambayo ilitumia pauni £2.5 katika kipindi kilichopita sasa imepanda kwa asilimia 300% kuwalipa mawakala ambapo hesabu zinaonyesha kuwa klabu hiyo imetumia pauni milioni £6.8 kuwalipa watu wa kati.

Usajili wa wachezaji kama Julio Cesar, Jose Bosingwa na Djibril Cisse kule Loftus Road katika kipindi cha miezi 12 iliyopita umewagharimu sana lakini pamoja na matumizi hayo bado klabu hiyo inaburuza mkia wa ligi ikiwa katika umbali wa alama 8 kutoka mstari wa hatari ya kushuka daraja.

Klabu ambayo imeonyesha kutumia kiasi kidogo kuwalipa mawakala ni Southampton, ambayo ni klabu pekee inayoshirikia Premier League iliyofanya matumizi chini ya pauni milioni £1.

Jumla ya pesa zilizo tumiwa na vilabu vyote 20 kufanya matumizi ya malipo ya mawakala katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita imepanda kufikia zaidi ya pauni milioni £77 tofauti na kipindi kilichopita cha Oktoba 2010 mpaka septemba 2011.

Kiasi kilichotumiwa na kila klabu kuwalipa mawakala Oktoba 2011 mpaka Septemba 2012 ni kama ifuatavyo

Manchester City - £10,537,982
Liverpool - £8,600,444
Queens Park Rangers - £6,818,688
Tottenham Hotspur - £6,595,905
Chelsea - £6,490,382
Arsenal - £5,580,873
West Ham Utd - £4,436,992
Manchester Utd - £3,681,580
Newcastle Utd - £3,485,503
Everton - £3,092,891
Aston Villa - £2,730,539
Fulham - £2,581,208
Sunderland - £2,173,762
Reading - £2,167,833
Wigan Athletic - £1,974,305
Stoke City - £1,717,266
West Bromwich Albion - £1,341,301
Norwich City - £1,248,725
Swansea City - £1,100,845
Southampton - £646,106

No comments:

Post a Comment