Timu ya
taifa ya Tanzania Bara The Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga katika hatua
ya robo fainali ya michuano mataifa ukanda wa Afrika mashariki na kati maarufu
kama michuano ya Chalenji kwa ushindi wa karamu baada ya kuichapa Somalia kwa
mabao 7-0.
Mchezo huo
kwa timu zote mbili ulikuwa ni mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wakiwa
katika kundo la B mchezo uliochezwa katika viwanja vya KCCA ulioko Lugogo.
Mrisho
Ngassa ya kukandamiza goli 5 huku John John
Raphael Bocco akifunga magoli mawili.
Ngasa
alianza kuandika bao la kwanza kunako dakika ya kwanza ya mchezo na kuanza
kuamsha furaha za mashabiki kabla ya kuandika bao la pili kunako dakika ya 24 na
baadaye John Bocco kuandika bao la tatu kunako dakika ya 27 na lingine kunako
dakika ya 42.
Dakika moja
kabla ya mchezo huo kwenda mapumziko Ngasa tena akaandika bao la tano na kuwa
mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu ndani ya mchezo mmoja ‘hat trick’
katika michuano ya mwaka huu.
Baada ya
mapumziko wasomali walijaribu kuzui lakini juhudi zao hazikua dafu pale Ngassa aliandika
bao la nne na la tano kwa Kilimanjaro katika dakika za 73 na 75th.
Huo ndio
ushindi mkubwa tangu michuano hiyo kuanza.
Mabao hayo
matano ya Ngasa yanamfanya kuwa ndiye mfungaji anayeongoza mpaka sasa kwa
kufunga magoli mengi huku John Bocco akimfuatia akiwa na magoli manne.
Wakati Burundi
wakikamilisha kwa ushindi wa bao 1-0 idi ya Sudan, Kilimajaro stars sasa
itakuwa imemaliza hatua ya makundi ikishika nafasi ya pili na sasa ikitarajiwa
kukutana na Rwanda katika hatua ya robo fainali.
Katika michezo
ya kundi la C Malawi imefanikiwa kuifunga Zanzibar kwa mabao 2-0 mchezo
uliochezwa katika uwanja wa Wankulukuku.
Mabao ya
Malawi yamefungwa na Ndaziona Chatsalia na Chiukepo Msowoya yakifungwa katika dakika za
mapema.
Malawi
imemaliza ikiwa katika nafasi ya pili katika kundi hilo ambalo limeongozwa na
Rwanda baada yah ii leo kuichapa Eritrea kwa mabao 2-0.
Kwa upande
wao Burundi wao wamewachapa Sudan kwa bao 1-0 mchezo uliofanyika katika uwanja
wa at Wankuluku. Bao la washindi lilifungwa Chris Nduwagira kunako dakika ya 16
na hivyo Burundi wakimaliza hatua ya makundi bila ya kufungwa.
No comments:
Post a Comment