KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, December 2, 2012

HILA ZA WAKONGO BRAZZAVILLE ZAWASAIDIA KUYEYUSHA NDOTO ZA WATANZANIA KUCHEZA FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA KWA VIJANA WA U-17 MOROCCO.

Taarifa zilizoifikia Rockersports zinasema kuwa timu ya taifa ya Vijana ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys imeishindwa kufuzu fainali ya mataifa ya Afrika kwa vijana ambayo itafanyika nchini Morocco mwezi machi mwakani baada ya hii leo kufungwa kwa mabao 2-0 na wenyeji Congo Brazzaville.

Mchezo huo ulikuwa ni wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita ambapo Serengeti iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.

Kabla ya mchezo huu wa marudiano Serengeti ilikuwa ikihitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kuweza kufuzu.

Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kulikuwepo na mazingira ya vurugu zilizo andaliwa na wenyeji za makusudi  kabla ya mchezo na hata wakati wa mchezo ambazo ziloiiathiri wachezaji wa Serengeti ikiwemo kupigwa na askari wa jeshi la polisi kwa kocha msaidizi  Jamhuri Kihwelu Julio kipigo ambacho haikujulikana mara moja kilitokana na nini.

Hila na vituko kwa benchi la ufundi na wachezaji wa Serengeti vilitawala vilitawala katika sehemu kubwa ya mchezo ndani na nje ya uwanja kwa lengo la kumghadhibisha Jamhuri Kihwelu na wengine na hatimaye askari kutumika kwenda kumchapa Kihwelu.

Kabla ya mchezo pia meneja wa Serengeti naye alipigwa huku sababu ya kipigo kushindwa kujulikana.

Rockersports imezungumza na katibu wa shirikisho la soka nchini Angetile Oseah ambaye amesema walikuwa wakiwasiliana na viongoxi walio ambatana na kikosi hicho ili kujua nini kilitokea kabla, wakati wa mchezo na baada ya mchezo ndipo atakapo weza kutoa taarifa kwa umma.

Kama itakumbukwa katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa taifa mwamuzi wa mchezo ule alimtoa nje ya uwanja kocha wa timu ya vijana ya Congo Brazzaville jambo ambalo lilionekana kuwakasarisha wacongo hao ambao waliapa kulipiza kisasi timu hiyo itakapo elekea kwao yakiwa ni maneno yaliyotamkwa na kocha msaidizi baada ya mchezo.

Kitendo kilichotokea katika mchezo huu wa marudiano kinaweza kutafsiriwa kama ni ulipaji wa kisasi wa makusudi kwa Serengeti Boys.

No comments:

Post a Comment