Wenyeji wa
michuano ya Confideration Cup Brazil wamepangwa katika kundi moja na Japan,
Mexico na Italia katika kundi la ufunguzi wa michuano ya Confederations Cup.
Mabingwa wa kombe la dunia na Ulaya Hispania atakuwa katika kundi moja la
B pamoja na nchi za Uruguay na Tahiti pamoja na mshindi wa fainali ya mataifa ya Afrika ambaye
atajulikana mwezi Februari.
Michuano hiyo
hufanyika kila baada ya miaka minne na kushindanisha mabingwa wa kila bara.
Rais wa
shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amepongeza miundo mbinu ya nchi
mwenyeji wa fainali hizo Brazil.
Amenukuliwa akisema,
"Mambo
mengi yamebadilika katika nchi hii tangu mwaka 1950, Brazil imeendelea sit u katika
eneo la utamaduni lakini pia hata katika uchumi”.
Rais wa Brazil
Dilma Rousseff pia alikuwepo katika droo hiyo ambapo amesisitiza kuwa viwanja
vitakuwa tayari mpaka kufikia wakati ya michuano hiyo.
Benitez ajitambua si wa asilimia 100% kupona darajani.
Rafael
Benitez ameweka wazi kuwa hana uhakika na nafasi yake ya kazi kuwa salama
kufuatia ndoto yake ya kuanza maisha mapya Chelsea kukumbwa na bahati mbaya
baada ya kichapo kutoka kwa West Ham cha mabao 3-1.
Hiyo ina
maana kuwa Chelsea sasa imecheza michezo saba bila ushindi katika ligi kuu ya
soka nchini England ‘Premier League’.
Benitez bado
anasaka ushindi wa kwanza akiwa ndio kocha wa kwanza chini ya utawala wa
mmiliki Roman Abramovich kushindwa kupata ushndi katika michezo miwili ya
kuanza kazi yake.
Benitez
amekuwa akikumbana na kelele za mashabiki wenye hasira ambao wamekuwa
wakionyesha waziwazi hisia zao kwa kutoa maneno na kuandika kwenye mabango
"You're not welcome here'' na nyimbo zikiimbwa yakitamkwa maneno
"You're
getting sacked in the morning".
Benitez yuko
katika hali tete kufuatia kuanza kuulizwa juu ya uwezo wake na mmiliki Roman
Abramovich ambaye anaonekana kama mmiliki asiyekuwa na subira.
Alipoulizwa kama
ana hofu yoyote juu ya uwezekano wa kuondoka Stamford Bridge ndani ya kipindi
kifupi, Benitez ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu amesema,
"ningependa kusema kuwa inategemea na
mambo yatakavyo kuwa uwanjani. Kwahiyo kama tuta ongeza juhudi uwanjani itakuwa
rahisi kwa kila mtu''
Wenger naye hana amani Emirate
Arsene
Wenger amesema atafanya tathmini juu ya hatma take ya baadaye katika klabu ya Arsenal
baada ya msimu kumalizika kufuatia kufanya vibaya dhidi ya Swansea City ambapo
walifungwa bao 2-0.
Mabao mawili
ya dakika za mwisho yaliyofungwa na Michu yameifanya Arsenal kupoteza sasa
jumla ya minne na kuiweka katika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi baada
kushuka uwanjani mara 15.
Alikuwa akizomewa
na baadhi ya mashabiki kutoka upande mmoja wa uwanja wa Emirates hapo jana sambamba
na kukumbwa na upinzani na kundi la 'Black Scarf Movement' ambao wana hasira na matokeo mabovu yanayoendelea kwa timu yao.
Baada ya
kupoteza mchezo huo, Wenger aliulizwa kama bado ana hamu ya kuendelea kuishikilia nafasi hiyo
ambayo amekuwa nayo tangu mwaka 1996, amejibu,
"hapana,
unafanya tathmini mpaka mwisho wa msimu. Najua hali imetibuka kila upande. Ni wakati
sasa wa kuungana pamoja na kuonyesha kuwa ni klabu imara"
Alipoulizwa kama
anaumizwa na timu hiyo katika hatua hii kuwa katika nafasi ya katikati ya
msimamo wa ligi , Wenger amesema
“Ni kweli. Lakini siogopi kuwepo katika nafasi
hiyo. Tunatakiwa kupata ubora tena".
No comments:
Post a Comment