Michuano ya kombe la dunia ya mwaka wa 2022 nchini Qatar inaendelea
kugonga vichwa vya habari kutokana na sababu chungu nzima, na bodi ya
maamuzi ya FIFA imekutana ili kulijadili kwa mapana
Pamekuwa na pendekezo la kutaka kuhamisha michuano hiyo kutoka miezi ya
majira ya joto, ili kuwaepusha mashabiki na wachezaji dhidi ya joto
kali…
Na baada ya mkutano wa jana, Rais wa FIFA Sepp Blatter ametangaza kuwa
michuano hiyo itaandaliwa nchini Qatar kama ilivyopangwa, lakini uamuzi
kama kweli itaandaliwa katika majira ya joto utafanywa baada ya dimba
la kombe la dunia nchini Brazil. Amesema jopokazi(taskforce) litashauriana na
viongozi wa kabumbu na kampuni za matangazo kote ulimwenguni, na kisha
kuwasilisha ripoti yake kwa kamati kuu baada ya miezi kadhaa.
Bodi ya Blatter pia inatafuta jibu kuhusu unyanyasaji
unaofanywa na Qatar dhidi ya wafanyakazi ambao ni wahamiaji, baada ya
kutokea madai ya vifo na ukiukaji wa haki za binadamu katika miradi ya
ujenzi wa viwanja vya michezo itakayotumika kwa dimba hilo la dunia.
Blatter amekuwa akiishawishi FIFA katika miezi ya karibuni, kutaka
kubadilisha tarehe za dimba la dunia la 2022…Kamati Kuu ya Qatar 2022
inasisitiza kuwa inaweza kuandaa dimba lililo salama, mwezo Juni na
Julai, kwa kutumia tekonolojia ya hewa ya baridi, ijapokuwa itatii amri
kama FIFA itaafikiana kwa kauli moja kubadilisha tarehe hizo.
Changamoto za kisheria katika uamuzi wa kuzibadilisha tarehe za dimba
hilo zimekuwa zikizungumziwa kwa muda mrefu na nchi zilizoshindwa kupewa
haki za kuliandaa, ligi za soka Ulaya zikilazimika kubadilisha ratiba
zao za Agosti hadi Mei nazo kampuni za matangazo zikilazimika kununua
haki za kurusha matangazo kwa tamasha hilo la Juni hadi Julai.
No comments:
Post a Comment