Hatimaye meneja wa Manchester United, David Moyes, amekiri kuongoza
miamba hao wa Uingereza ni kibarua kigumu kuliko vile alitarajia.
Taarifa hiyo inatia shaka kubwa kuwa meneja huyo aliyetoka Everton hana
uwezo wa kumudu hadhi ya kuwaongoza mabingwa hao mara 20 wa taji la ligi ya
Uingereza.
Akizungumuza baada ya kupoteza mechi yake ya tano nyumbani katika
Premier musimu huu mikononi mwa waasimu wao wa jadi, Liverpool, Moyes
alikubali kwamba kibarua cha United kimekuwa changamoto ambayo
hakukisia.
“Kazi ikikuwa ngumu kutoka mwanzo. Lakini imekuwa ngumu zaidi ya nilivyotarajia,” Moyes alikiri.
“Hilo linaonyesha kuwa hatupati matokeo yanayostahili. Ni lazima
tucheze vyema zaidi ili iwe ni vigumu kututawala huku tukihakikisha ya
kwamba tunabuni nafasi na kufunga mabao zaidi.”
United wanadorora katika nafasi ya saba, alama 18 nyuma ya vingozi
Chelsea baada ya kushinda ligi hiyo na mwanya wa pointi 11 musimu jana.
No comments:
Post a Comment