Mshambuliaji wa PSV Eindhoven Zakaria Bakkali bado kuamua kuichezea timu ya taifa ya Morocco licha ya kutajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Belgium ambayo inajiandaa kucheza michezo miwili ya kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia dhidi ya Croatia Scotland.
Mzaliwa huyo wa Belgium mwenye umri wa miaka 17 wazazi wake ni raia wa Morocca waliohamia Belgium lakini akiwa na uraia wa nchin mbili lakini mpaka sasa bado hajacheza nchi yoyote kati ya hizo mbili katika michuano ya timu za taifa za wakubwa na hivyo kuwa bado na uhalili wa kucheza upande wowote aupendao.
Akiongea na gazeti la kidachi la Algemeen Dagblad amenukuliwa akisema
"Kuna watu wengi wanazungunza kwa kunilisha maneno lakini mwenyewe bado sijaamua.
"Ni maamuzi magumu."
Bakkali mara mbili amekuwa akitajwa katika kikosi cha Belgium lakini bado kuichezea timu hiyo.
Endapo ataichezea katika mchezo mmoja wa kusaka kufuzu kombe la dunia basi moja kwa moja atakuwa amejihalalisha kimataifa na Belgium.
No comments:
Post a Comment