Kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'The Uganda Cranes' msebia Mulitin ‘Micho’ Sredojevic amefanya mabadiliko ya kikosi chake katika kikosi cha kwanza ambacho kilipokea kichapo kutoka kwa Misri cha mabao 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki hivi karibuni.
Msebia Micho ambaye kikosi chake kitakutana na Mafarao kwa mara ya tatu ndani ya kipindi kisicho zidi miezi miwili kiwaondoa kikosini kiungo wa SC Victoria University Manko
Kaweesa, mshambuliaji Simon Okwi na nyota wa URA FC Said Kyeyune na nafasi zao kuchukuliwa na Yusuf Mukisa,
Jonathan Mugabi na Simon Namwanja.
Katika kile kinachoonekana ni kuimarisha safu yake ya ulinzi kikiso cha kwanza kitakuwa na walizni Mukisa na Namwanja katika ulinzi wa pembeni ambao watakuwa wakichukua nafasi za Kisaliita na Majwega ambao walikuwepo kikosini jumatatu katika nafasi hizo.
Kisaliita sasa atakuwa akielekea sehemu ya kiungo wa kati ambapo atakuwa akishirikiana na mgeni kikosini Jonathan Mugabi wakicheza kama viungo wawili wachezeshaji "holding midfielders" huku Majwega akielekea upande wa kushoto kwa juu na Wadada akisalia katika winga ya kulia.
Mshambuliaji wa URA FC Frank Kalanda ambaye bado hajafunga goli katika klabu yake mpya atakuwa kisimama mbele akisaidiwa na kiungo wa Vipers SC
Joseph Mpande.
Mlinda mlango wa SC Victoria University Benjamin Ochan ataendelea kusalia katika milingoti kitatu huku Richard Kasagga na Savio Kabugo katika sehemu ya uklinzi wa kati.
Uganda imechapwa mara tatu na Misri na ikifungwa pia na Snegeal mara moja huku ikipata ushindi mchezo mmoja dhidi ya Botswana wakati huu ambapo inajiandaa kwa ajili ya michuano ijayo ya Cecafa Tusker Challenge 2013 ambayo itafanyika Novemba 27 mpaka Desemba 12.
Uganda pia inajiandaa kwa fainali ya michuano ya Chan mwezi Januari nchini Afrika kusini.
Zipo taarifa ambazo bado hazija thibitishwa kuwa Uganda na Misri watakutana tena kwa ajili ya mchezo mwingine wa kimataifa wa kirafiki ikiwa ni kipimo cha Misri kabla ya kukutana na Ghana mchezo wa kwanza kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia Oktoba 15.

KIKOSI KAMILI CHA UGANDA
Uganda XI: Benjamin Ochan (GK), Mukisa Yusuf, Ayub Kisaliita, Richard
Kasagga ©), Savio Kabugo, Simon Namwanja, Jonathan Mugabi, Nicholas
Wadada, Joseph Mpande, Frank Kalanda and Brian Majwega
Substitutes: Brian Bwete (gk), Simon Okwi, Said Kyeyune, Brian Nkuubi, Manko Kaweesa, Moses Feni Ali and Hassan Wasswa
No comments:
Post a Comment