Na Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MAKOCHA 32 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA COPA COCA-COLA
Makocha
32 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wanashiriki kozi ya Copa
Coca-Cola inayoanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam
chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa
Miguu (FIFA).
Kozi
hiyo itakayomalizika Agosti 17 mwaka huu itafunguliwa saa 3 kamili
asubuhi kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre na washiriki wote tayari
wameshawasili Dar es Salaam. Mkufunzi wa kozi hiyo ni Govinder Thondoo
kutoka Mauritius.
Washiriki
wa kozi hiyo ni Ahazi Ibrahim Kasegese (Mbeya), Aloyce Mayombo (Pwani),
Andrew Zoma (Tabora), Asuri Msakamali (Simiyu), Bakari Khamis Kilambo
(Kaskazini Pemba), Chacha Sambulo (Mara), Charles Rwezaura (Kagera),
Daniel Sambala (Njombe), Dudu Haruni (Iringa) na Emmanuel Kapurata
(Rukwa).
Faki
Makame Haji (Kaskazini Unguja), Fatawi Khamis Sheha (Kusini Pemba),
Hamisi Omary Mabo (Kigoma), Hussein Maulid (Morogoro), Issa Lugaza
(Kilimanjaro), James Gaspar (Shinyanga), James Wambura (Arusha), Jomo
Jackson Puccey (Lindi), Joseph Sihaba (Dodoma), Kelvin Haule (Ruvuma) na
Kessy Juma Abdallah (Tanga).
Kessy Mziray (Mwanza), Menswi Mchwampaka (Kinondoni), Mohamed Abdallah Kweka (Singida), Nurdin Gogola (Temeke), Pius
Kamande (Rukwa), Ramadhan Abrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Ramadhan
Salum Mnyoti (Manyara), Raphael Ngeleja (Geita), Samuel Edgar Maokola
(Ilala), Shaweji Nawanda (Mtwara) na Vuai Abdul Haji (Kusini Unguja).
Fainali za U15 Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa zitafanyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.
SEMINA YA MAKAMISHNA YAANZA DAR, MWANZA
Semina
kwa ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness
test) kwa waamuzi
wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha VPL msimu wa
2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) katika vituo vya Dar es
Salaam na Mwanza.
Mafunzo
hayo yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu yatakuwa chini ya wakufunzi
Leslie Liunda, Joan Minja na Riziki Majara kwa kituo cha Dar es Salaam
wakati kituo cha Mwanza kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde.
Kwa Dar es Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Kituo
cha Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita,
Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu,
Singida na Tabora.
Kituo
cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya
Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya,
Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment