Azam fc imefanikiwa kusonga mbele katika mzugnuko wa pili wa michuano ya vilabu barani barani Afrika kombe la shirikisho baada ya kuichapa Al Nasr ya Sudan kusini kwa mabao 5-0 jijini Juba nchini Sudan.
Huo ulikuwa ni mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Azam waliochomoza na ushindi wa mabao 3-1 na hivyo kuifanya Azam kuitoa Al Nasr kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1..
Katika mchezo wa leo mabao ya Azam yalitiwa kwenye kamba na Kipre Tcheche na John Bocco kila mmoja akifunga mabao mawili na bao la tano likifungwa na Mcha Hamisi 'Viali'
Kwa upande wao mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Simba waliokuwa nchini Angola wakicheza mchezo wa marudiano dhidi ya FC Libolo ya huko imeshindwa wameshindwa kukwepa mvua ya mabao, kufuatia kukumbana na dhahma ya kichapo cha mabao 4-0.
Itakumbukuwa katika mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Simba walikubali bao 1-0 ambalo liliondosha matumaini yao ya kusonga mbele tangu mapema.
Aidha matokeo ya kuondoshwa kwa mwakilishi huyo wa Tanzania katika mchuano ya vilabu bingwa barani Afrika yamepokelewa kwa masikitiko makubwa na mashabiki wa timu hiyo kongwe nchini.
Rockersports imeshuhudia mijadala mizito kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo, huku lawama nzito zikielekezwa kwa uongozi wa klabu hiyo kwa kushindwa kuweka mikakati thabiti ya ushiriki wa timu hiyo tangu mapema.
No comments:
Post a Comment