1. Liewig aahidi kupambana hadi mwisho
2. Poppe aahidi mamilioni kwa wachezaji
3. Kapombe asema Sunzu atawaua Waangola
Na Ezekiel Kamwaga, Kwanza Sul,
Angola
KOCHA
Mkuu wa Simba, Patrick Jean Elysee Liewig, amesema ana matumaini timu yake
itapata matokeo mazuri katika mchezo wa kesho baina ya Wekundu wa Msimbazi na
Libolo ya Angola.
Mechi
hiyo imepangwa kuchezwa kesho kuanzia saa tisa alasiri katika Uwanja wa Estadio
Libolo, uliopo katika mji mdogo wa Calulo jimbo la Kwanza Sul.
Katika
mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, Simba ilifungwa 1-0 na mabingwa hao wa
Angola.
Hata
hivyo, Liewig alisema ingawa matokeo ya kufungwa nyumbani hayakuwa mazuri, ana
imani Simba nayo inaweza kufanya vizuri ugenini.
“Kama
wao walitufunga kwetu kwanini sisi tusiwafunge kwao. Ukiangalia kwenye ile
mechi ya kwanza wao walipata nafsi moja tu ya maana na wakaitumia. Sisi
tulipata nafasi kama tatu hivi na hatukutumia vizuri hata moja,” alisema.
Liewig
alisema ameridhishwa na ari na mazoezi mazuri ambayo Simba imefanya kwa wiki
nzima kujiandaa na mechi hiyo na kwamba kuna dalili kuwa timu yake inaweza
kufanya lisilotarajiwa.
Akizungumza
na wachezaji katika kikao kilichofanyika katika Hoteli ya Anisaan Ritz ambako
Simba imefikia, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Zacharia Hans Poppe,
alitoa ahadi ya Sh milioni 10 iwapo watafanikiwa kuitoa Libolo.
Aliwataka
wachezaji wa Simba kuwakumbuka mamilioni ya washabiki wao waliopo Tanzania
ambão hawalali wala kula vizuri wakati timu yao kipenzi inapokuwa na matokeo
mabaya.
Poppe
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba na pia kundi la Friends
of Simba, alisema ana imani kubwa na wachezaji wa timu yake kwa vile ndiyo bora
Tanzania na kama wataamua kucheza kwa nguvu zao zote, matokeo mazuri
yanawezekana.
“Nyie
ni wachezaji wazuri sana. Kama nyote mtacheza kama timu na mkacheza kwa uwezo
wenu wote, ni wazi kwamba mnaweza kuibuka na ushindi,” alisema.
Akizungumzia
mechi ya kesho, nahodha msaidizi wa Simba, Shomari Kapombe, alisema mechi baina
yao na Libolo itakuwa tofauti na ya kwanza kwa sababu ya kuwepo kwa
mshambuliaji Mzambia, Felix Sunzu.
“Tulimkosa
sana Sunzu kwenye mechi ya Dar es Salaam. Mipira ilikuwa haikai kule mbele na
hilo lilikuwa tatizo kubwa, kubwa sana na hiyo ni kwa sababu Sunzu hakuwepo.
Nadhani sasa tuna nafasi zaidi kuliko mara ya kwanza,” alisema.
Mwisho.
Aliyechezesha Simba na Shandi
kuchezesha Libolo
Na
Ezekiel Kamwaga, Angola
MWAMUZI
Nhleko Simanga Pritchard kutoka nchini Swaziland ambaye alichezesha mechi baina
ya Wekundu wa Msimbazi na Al Ahly Shandi ya Sudan mwaka jana, ndiye
atakayechezesha mechi ya kesho dhidi ya Libolo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyopatikana kutoka Chama cha Soka cha Angola leo asubuhi,
mwamuzi huyo atasaidiwa na na wenzake Mkhabela Bhekisizwe, Mbingo Petros na
Fabudze Mbongiseni ambão wote wanatoka Swaziland.
Kati
ya hao, ni Nhleko na Petros pekee ambão ndiyo waliochezesha mechi ya Shandi
ambayo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na Haruna Moshi
(77), Patrick Mafisango ambaye sasa ni marehemu (88) na Emmanuel Okwi (90).
Wachezaji
wote hao watatu waliofunga katika pambano hilo hawatacheza katika mechi ya
Libolo kwa sababu tofauti. Mafisango alifariki kwa ajali siku mbili baada ya kurejea
kutoka Sudan kwenye mechi ya marudiano ambako Simba ilitolewa.
Okwi
amehamia katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na Boban ameshindwa
kusafiri na timu kwenda Angola kwa sababu ya kushikwa na malaria kali.
Kamisaa
wa pambano hilo lililopangwa kuanza majira ya saa tisa kamili kwa saa za hapa
(sawa na saa 11 jioni kwa saa za Tanzania) anatarajiwa kuwa Mandla Mazibuko
kutoka nchini Afrika Kusini.
Mwisho
Libolo yatumia uwanja kutafuta
ushindi
Mwandishi Wetu, Angola
BENCHI
la ufundi la Simba SC jana limeukagua Uwanja wa Estadio Libolo itakakochezwa
mechi ya kesho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Wekundu na Libolo na kubaini
siri nzito.
Vipimo
vya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig, vilibaini kwamba uwanja huo una
upungufu wa takribani mita sita kwa urefu na upana kulinganisha na viwanja
vingi vya soka.
Kwa
mujibu wa Liewig, uwanja huo umepunguzwa ukubwa ili kusaidia timu ya Libolo
ambayo inafahamika sana kwa kufunga mabao mengi ya mipira iliyokufa (adhabu,
kurusha n.k).
“Kutokana
na hali hii, maana yake ni kwamba kila itakapokuja kona, itakuwa hatari kwa
sababu kuna umbali mdogo kutoka kwenye kona hadi goli. Itakuwa hatari
hivyohivyo kwenye mipira ya kurusha na ya adhabu. Ni muhimu tumeliona hili
mapema,” alisema.
Alisema
atawaeleza wachezaji wake kujiepusha kutoa kona au mipira ya kurusha bila ya
sababu kwa vile inaonekana hiyo ndiyo silaha kubwa ya wapinzani hao wa Simba.
“Kama
unakumbuka, hata goli lao la Dar lilitokana na mpira wa kurusha halafu ikapigwa
krosi. Ndiyo maana nafikiri wameleta mechi hii huku badala ya Luanda ili
watumie faida hii vizuri,” alisema.
Nchini
England, Uwanja wa Britannia unaotumiwa na timu ya Stoke City inayocheza Ligi
Kuu ya nchi hiyo unafahamika pia kwa kuwa mdogo kwenye eneo la kuchezea kuliko
viwanja vingi vya nchi hiyo.
Hata
hivyo, inaelezwa kwamba lengo kuu la kuuweka uwanja huo katika eneo hilo ni
kutumia nguvu ya mipira ya kurusha na adhabu nyingine ambayo ndiyo silaha kubwa
ya Stoke. Miaka miwili iliyopita, robô ya magoli yaliyokuwa yakifungwa na timu
hiyo yalitokana na mipira ya kurusha ya Rory Delap
No comments:
Post a Comment