Ghana ilipiga hatua kubwa katika kufikia
kinyang'anyiro cha kombe la dunia baada ya kuicharaza Misri mabao 6-1
katika mkondo wa mwisho wa mechi za kufunzu kwa kombe la dunia mwaka
2014 nchini Brazil.
Asamoah Gyan aliingiza bao la kwanza ambalo lilifuatiwa na lengine la mchezaji wa Misri Wael Gomaa katika lango la Ghana.
Mchezaji wa Misri, Mohamed Aboutrika
aliingiza bao la penalti lakini Gyan akaingiza bao lengine na kuyafanya
matatu dhidi ya moja kabla ya kipindi cha mapumziko.
Bao lengine la penalti liliingizwa na Sulley Muntari na kuyafanya manne.
Christian Atsu naye alipata fursa na kuopnyesha
nyota yake kwa kuingiza bao lengine huku akiiweka Ghana kifua mbele na
kudhibiti mechi.
Mechi hiyo, ilikuwa imesemekana kuwa ngumu kwani timu hizo mbili zina wachezaji wazuri sana
Lakini kwa sasa ni kama wazi kuwa Black Stars wa
Ghana wataabiri ndege ya kwenda Brazil baada ya ushindi wao mkubwa
mjini Kumasi.
Hali ya wasiwasi ilijitokeza kabla ya mechi huku
Ghana ikilalamikia FIFA kuwa inahofia kucheza mechi hiyo mjini Cairo
kutokana na hali ya kisiasa ilivyo nchini Misri.
Huku ikiwa bado haijulikani mechi ya marudio
itakochezwa, nia ya Ghana ilikuwa kupata alama nzuri zaidi ya Misri,
nyumbani na hivyo ndivyo ilivyofanyika.
No comments:
Post a Comment