Katika
hali isiyokuwa ya kawaida,Mashabiki wa timu ya Simba hii leo kwa mara nyingine tena wameng'oa viti vya kukalia uwanja wa taifa na kuwatupia Mashabini wenzao wa
Timu ya Yanga waliokuwa wamefurika uwanja wa taifa kwa kile kinachodaiwa
kuwa hawataki kukaa nao sehemu moja.
Uongozi wa Vilabu hivi viwili vikubwa hapa nchini, shirikisho la soka pamoja na serikali wanatakiwa kukaa
chini na Mashabiki hao na kuwakanya kuhusiana na uharibifu wa
Miundombinu wanaoufanya na mashabiki hao huku adhabu kali ikibidi kwenda mahakamani kujibu mashitaka ikiwa ni pamoja na kulipa fidia.
Mpira wa miguu hauwezi kuendelea kwa kuharibu miundo mbinu ya mpira iliyojengwa kwa gharama kubwa huku wadau hao muhimu wakitazama, hivi ni vitendo vya hovyo vinavyotakiwa kutafutiwa ufumbuzi haraka endapo kweli kama taifa linataka kunusuru maswahibu mengine makubwa ambayo yanaweza kutokea hapo baadaye.
Mashabiki
wa Timu ya Simba wakiendelea kuwarushia viti Mashabiki wa timu ya Yanga
kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza uwanjani hapa.
Viongozi
wa timu ya Yanga wakiwaomba Mashabiki wao kuhama katika eneo hilo na
kwenda kujibana katika eneo walilotengewa kama wana Yanga.
Mashabiki wa timu ya National Al Ahly wakiongea na Askari Polisi kuomba wakalizuie tatizo hilo.
Askari
Polisi wakiongea na Viongozi wa Timu ya Yanga ili waweze kwenda
kuwaomba mashabiki wao waaondoke katika upande ule unaodaiwa kuwa ni wa
Mashabiki wa Simba.
Mambo yalianza kama masihara huku wengine wakitaniana kabisa. |
No comments:
Post a Comment