Kikosi
cha wachezaji 25 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka
17 (Serengeti Boys) kimeingia kambini leo (Oktoba 21 mwaka huu) jijini
Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya raundi ya mwisho ya michuano ya
Afrika kwa vijana.
Serengeti
Boys ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen itacheza mechi hiyo ya
raundi ya tatu na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Zimbabwe ambapo
tayari Congo Brazzaville imefanikiwa kupata ushindi wa ugenini wa mabao
2-1. Mechi ya marudiano itachezwa jijini Brazzaville kati ya Oktoba
26-28 mwaka huu.
Katika
mechi hiyo ya raundi ya tatu, Serengeti Boys itaanzia nyumbani katika
mchezo utakaofanyika Novemba 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, wakati
mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liko katika mikakati ya kuhakikisha
Serengeti Boys inapata mechi mbili za kirafiki za kimataifa kabla ya
kumvaa mshindi kati ya Congo Brazzaville na Zimbabwe. Fainali za Afrika
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika Machi mwakani nchini
Morocco.
No comments:
Post a Comment