Wakati
kiungo mwenye uwezo wa kucheza kama kiraka Mkongo Mbuyu Twite akiendelea kutimiza wajibu wake wa kuitumikia
klabu ya Yanga tena kwa kiwango safi, pacha wa kiungo huyo Kabange Twite
amewasili nchini na jana alikuwepo katika uwanja wa Taifa akimshuhudia pacha
wake Mbuyu akisukuma gozi na cha kufurahisha akifunga bao la kwanza katika
mchezo dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Taifa.
Akiongea na
Rockersports Kabange amesema kimsingi amekuja nchini kumtembelea pacha wake
ambaye amekuwa mbali naye kwa muda tangu ajiunge na Yanga.
Kama
Itakumbukwa kabla ya kujiunga na Yanga Mbuyu pamoja Kabange wote walikuwa wamemaliza mikataba
yao na klabu ya APR ya Rwanda na moja ya masharti ya ndugu hao ilikuwa ni
kujiunga na ama Simba au Yanga wakiwa pamoja vilabu ambavyo vilikuwa vitani kutaka
saini zao kabla ya Mbuyu aliyekuwa kivutio katika michuano ya Kagame kujiunga
na Yanga.
Akiongea na
Rockersports Kabange amesema hayuko tayari kuzungumzia juu ya hilo licha ya
kukiri kuwa safari yake ya kuja nchini ilikuwa chini ya mmoja wa kigogo wa
klabu hiyo Abdalah Bin Kleb.
Rockersports
ilikuwa ikifanya naye mazungumzo wakati akimsubiri Bin Kleb kabla ya Bin Kleb
kufika na kuondoka naye katika ndinga la Kigogo huyo wa Yanga.
No comments:
Post a Comment