AC Leopards imekuwa
ni klabu ya kwanza kutoka Congo Brazzaville kutinga nusu fainali ya michuano ya
Confederation barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Djoliba
ya Mali mchezo ulichezwa Jumapili.
Leopards, yenye
maskani yake katika mji wa magharibi wa Dolisie, walihitaji matokeo ya kama ya Wydad
Casablanca ya Morocco katika dimba la Stade Malien kule Mali kujihakikishia
usalama wa nafasi ya pili nyuma ya washindi wa kundi B Djoliba.
Casablanca ilikwenda
sare ya bao 3-3 Stade baada ya kuwa na kazi ya kusawazisha mara tatu wakitokea
nyuma kimatokeo.
Historia inaonyesha
kuwa hakuna klabu kutoka Afrika ya kati iliyokaribia kushinda taji hilo tangu
CARA ya Brazzaville kufanikiwa kufanya hivyo mara ya mwisho 38 iliyopita.
Gedo aiongoza Al Ahly kutinga fainali ya mabingwa Afrika
Bao la
kipindi cha kwanza kupitia kwa Gedo lilitosha kuwapa ushindi Al Ahly na kutinga
fainali ya vilabu bingwa Afrika baada ya kigogo hicho cha soka barani Afriaca
kuichapa Sunshine Stars ya Nigeria.
Ushindi huo
wa Ahly wa bao 1-0 umewapa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 na sasa wanatarajia
kukutana dhidi wapinzani wao wakubwa katika ukanda wa kaskazini Esperance mwezi
ujao.
Bao lilitoka
na mpira wa shuti uliompoteza mlinda mlango Moses Ocheje kunako dakika ya 28 na
hivyo kukamilisha safari ya fainali ya Ahly baada ya mchezo wa kwanza
kumalizika kwa sare ya bao 3-3 nchini Nigeria wiki mbili zilizopita.
Mchezo huo
ulichezwa bila ya watazamaji kwa sababu za kiusalama baada ya vurugu za mwezi
wa pili ambapo pia Ahly ilitawala mchezo
katika sehemu kubwa ya mchezo huo.
Gerrard: Namkubali Sterling anaweza kufiki
mbali
Nahodha wa Liverpool
na timu ya taifa ya England Steven Gerrard anadhani Raheem Sterling anaweza
kufika mbali kimafanikio baada ya kuanza vizuri katika uchezaji wake timu za
wakubwa.
Kinda huyo
mwenye umri wa miaka 17 alifunga goli lake la kwanza kwa Liverpool mwishoni mwa
juma katika mchezo dhidi ya Reading, na kuwa mchezaji wa pili chipukizi katika
historia ya Liverpool kufunga goli.
Amenukuliwa Gerrard
akisema
"nadhani
ni mtu anaye mshangaza kila mtu, si kwasababu anafanya vizuri katika kiwango
hiki lakini pia hakuna anayedhani kuwa uwezo wake utakwisha mapema, nafikiri
kila mtu anajua kuwa ndio kwanza anaanza kuchezea timu ya wakubwa wakati
mwingine inabidi kuwa mwangalifu”
Gerrard
anaamini kuwa Brendan Rodgers ana imani na Sterling na kwamba ana kuwa ni
sehemu muhimu katika maendeleo yake lakini pia Gerrad akaonya kuwa kocha huyo
wa zamani wa QPR bado anasafari ndefu.
No comments:
Post a Comment