Kocha wa Ajax Frank de Boer amesema kikosi chake kinapaswa kuwaheshimu na sio kuiogopa Barcelona"respect, but not
fear" wakati wakijiandaa kukutana na wapinzani wao hao katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya katika dimba la Amsterdam ArenA hapo kesho Jumatano.
Wadachi hao walichapwa bao 3-1 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza mwezi uliopita na De Boer anasema hawataweza kurudia tena mwanzo huo mbaya.
Akiongea katika mkutano waanahabari amesema
"tunachopasw kufanya ni kucheza na kuwa na mpira wakati wote, tunapaswa kuwa makini zaidi tangu mwanzo wa mchezo kitu ambacho ni muhimu katika mchezo huo.
Huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa Luis Suarez kuichezea Barcelona
katika ligi ya mabingwa Ulaya atakapo kuwa dimbani Amsterdam ArenA Jumatano ya kesho kuvaana na Ajax katika mchezo wa kundi F.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliwahi kuichezea Ajax
frontman kwa miaka mitatu na nusu kwa mafanikio kiasi kuwa mchezaji bora mara mbili wa Ajax kabla ya kuelekea Liverpool mwaka 2011
No comments:
Post a Comment