KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, June 17, 2012

Messi athibtisha na kuvunja ukimya kuhusu mimba:nadhani atakuwa wa kiume


Mshambuliaji wa timu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Mess amevunja ukimya baada ya kutabiri na kuthibitisha kuwa mpenzi wake wa huenda akamzalia mtoto baada ya wiki kadhaa za tetesi kuwa mpenzi wake huenda amekuwa na ujauzito.
Mara kadhaa amekuwa akikwepa kujibu maswali ya wanahabari juu ya tetezsi hizo kuwa anategemea kupata mtoto wa kwanza na mpenzi wake Antonella Roccuzzo, hususani baada ya kufunga goli wa ushindi wa wa timu ya taifa ya Argentina wa mabao 4-0 dhidi ya Ecuador mapema mwezi huu.
Hatimaye ametangaza hadharani kuwa ni kweli mpenzi wake huyo ni mjauzito na kwenda mbali zaidi kwa kutabiri kuwa atakuwa wakiume.
"nadhani atakuwa wa kiume hatukutaka kusema lolote juu ya hilo kwakuwa hakuwahi kuzungumza lolote huko nyuma juu ya maisha yetu binafsi lakini tumekuwa kila siku tunajiuliza juu ya ya hili tunataka kuunganisha furaha yetu"
Haya habari ndi hiyo mshindi mara tatu wa Ballon d'Or akiichezea mara zote Argrntina tangu mwaka 2004, na mfungaji wa mabao 73michuano mbalimbali msimu uliopita sasa ni baba mtarajiwa.

No comments:

Post a Comment