KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, June 17, 2012

TAIFA STARS:Lakuvunda halina ubani.

Haya ndiyo machinjio ya Stars huko Msumbiji
 Hatimaye limedhihirika la msemo wa kiswahili wa la kuvunda halina ubani kufuatimu timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kuondoshwa katika kampeni za kuwania tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Mozambique mchezo ulichezwa mjini Mputo wakiondoshwa kwa njia ya mkwaju wa penati.

Mpaka dakika 90 za kawaida timu hizo zilikuwa zimekwenda sare ya kufungana bao 1-1 na hivyo kulazimika mchezo huo kuongezwa muda na hata baada ya muda wa ziada wa dakika 30 bado hali ilikuwa ngumu.
Mchezo huo ulipoingia katika hatua ya penati tano kila timu ilipata penati tatu wachezaji wawili wa Taifa Stars walikosa ni Aggrey Morris na Kelvin Yondani huku Amir Maftaha ,Shabani Nditi na Shomari Kapombe wakipata.
Baadaye zikaongezwa penati nne waliopiga na kupata ni John Boko ,Dumayo na Ngasa wakipata lakini Mbwana Samatta akakosa baada ya penati yake kudakwa na mlinda mlango wa Msumbiji.
Timu hiyo itarejea nyumbani Jumanne.

kikosi cha Stars kilicho kuwepo Msumbiji

No comments:

Post a Comment