KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, June 18, 2012

Yann M’Vila: ningependa kujiunga ligi ya Uingereza na hasa Arsenal

Kiungo mfaransa Yann M'Vila ametanabaisha kuwa ana hamu ya kuchezea ligi kuu ya nchini Ufaransa na haitakuwa rahisi kuacha nafasi ya kuelekea katika klabu ya Arsenal majira haya ya kiangazi endapo itatokea wanamtaka.
Washika mitutu hao walikuwa wakihusishwa na kutaka saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa lakini haija julikana kama wanajianda kukutana na klabu yake ya Rennes iliyokuwa ikihitajia euro milioni 20 kwa timu yoyote inayomtaka kinda huyo mahiri katika kusakata soka.
Lakini wakati hayo yakiwa hivyo mchezaji huyo mwenyewe mwenye kiungo mwenye umri wa miaka 21-hajaonekana kupingana na maamuzi ya kuuzwa kwake kuelekea katika klabu hiyo yenye maskani yake “Emirates Stadium” na ameonyesha kiu kubwa ya kutaka kuichezea ligi kuu ya nchini Uingerezamaarufu kama “Premier League”.
Amenukuliwa na Sporting Life akisema
"nimesikia kuhusu Arsenal kunitaka, naipenda Arsenal na naipenda Premier League.
"sijui nini kinatokea kati ya vilabi hivi lakini ndio ningependelea kuelekea Premier League na hasa Arsenal."
Klabu hiyo ya Arsenal toka London pia imekuwa ikimuwania mchezaji mwenzake wa timu moja na M’Vila’ huyu ni Olivier Giroud ambaye amekuwa kipenzi wa mashabiki wa klabu ya Montpellier.
M’Vila amekuwa akicheza katika ligi ya Ufaransa ya Ligue 1 akiwa na Rennes tangu alipokuwa na umri wa miaka 14, na amekuwa akiitumia klabu hiyo katika kikosi cha kwanza kwa zaidi ya michezo 100.

No comments:

Post a Comment