Taasisi inayopambana na ubaguzi wa rangi wa 'Kick It Out' imelitahadharisha jeshi la polisi juu ya ujumbe wa kibaguzi wa rangi kupitia akaunti ya twitter ya kiungo wa Manchester City Yaya Toure baada ya mchezo wa Jumapili dhidi ya wapinzani wao wa jiji la Manchester Manchester United.
Kiungo huyo alilazimika kuufunga kwa muda ukurasa wake huo kabla ya kurudishia uhai Jumatatu ikiwa ni siku moja baada ya mchezo wa ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast aliandika katika ukurasa wake huo
"Great to be back on Twitter after a good win
yesterday. Now my focus is on the next game...Happy Monday everyone!!"
Katika taarifa yake Jumanne ya leo, Kick It Out imesema kuwa Toure alipokea ujumbe wa kumbagua muda mfupi baada ya kutupia ujumbe ambapo ulionekana kuwakwaza baadhi ya wanaomfuata.
Msemaji wa Kick It Out amesema "tumepokea malalamiko kutoka katika jumbe mbili za tweeter zikimdhihaki kwa rangi Yaya Toure usiku wa jana.
"tumewaarifu polisi kupitia 'True Vision', kwa njia ya mtandao na tayari wamewatahadharisha Twitter.
No comments:
Post a Comment