Bosi wa ArsenalArsene Wenger anasema Rafael Benitez alikuwa na wakati mgumu sana alipokuwa na Chelsea lakini anaamini historia itadhihirisha kuwa alifanya kazi nzuri ndani ya klabu hiyo.
Benitez ambaye kwasasa ana umri wa miaka 53, atakuwa na kikosi cha Napoli huko London hapo kesho watakapokuwa wakikabiliana na washika bunduki wa Arsenal katika mchezo wa vilabu bingwa Ulaya.
Mhispania huyo alikuwa katika kipindi cha muda cha kukiongoza kikosi cha Chelsea tangu Septemba mwaka jana na kukiongoza mpaka kutwaa taji la michuano midogo ya Ulaya ya Europa lakini alishindwa kukubalika na kundi fulani la mashabiki wa klabu hiyo.
Alipoulizwa kama hakutendewa mema ndani ya Chelsea, Wenger alijibu "Yes."na kuongeza
"Watu walikuwa wagumu kwake kwasababu hawakutegeme yeye kuwepo Chelsea lakini alifanya vizuri. Aliwafanyia vema.
"Mwisho wa siku, watakubali kuwa alifanya vizuri."
- REKODI YA BERNITEZ.
- Valencia: La Liga (2001-02, 2003-04); Uefa Cup (2003-04)
- Liverpool: FA Cup (2005-06); Community Shield (2006); Champions League (2004-05); Uefa Super Cup (2005)
- Inter Milan: Supercoppa Italiana (2010); Fifa Club World Cup (2010)
- Chelsea: Europa League (2012-13)
Benitez, ambaye aliingoza Chelsea kushika nafasi ya tatu katika ligi kuu ya England 'Premier League', aliondoka Stamford Bridge na kwenda kuifundisha FC Napoli mwezi Mei.
Kesho atakuwa akikiongoza kikosi hicho kutoka Italia katika kukabiliana na Arsenal inayoongoza ligi ya England huu ukiwa ni mchezo wa kundi F katika michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment