Jose Mourinho amemchana meneja wa Arsenal Arsene Wenger baada ya meneja huyo wa Arsenal kulalamika kuwa uhamisho wa kiungo Juan Mata kujiunga na Manchester United si sawa"unfair"
Wenger amekuwa akiumizwa na uhamisho huo kwasababu Mata ataweza kucheza katika mchezo wa United dhidi ya Chelsea ambao ni wapinzani wao wa taji lakini na si kwa Blues pekee.
Hata hivyo Mourinho ameseka
"Kulalama kwa Wenger ni jambo la kawaida kwasababu ndivyo alivyozoea ni kitu ambacho tunakijua" .
"Kama Wenger akimuuza [Mesut] Ozil kwenda Man United nitafurahi sana kwasababu atakuwa amepoteza mchezaji mzuri lakini inawezekana Wenger kweli kulalamika na kusema it's not
fair.
Mata anatarajiwa kusafiri kwa Helikopta kuelekea uwanja wa klabu yake mpya wa Carrington baadaye hii leo na kukamilisha uhamisho wa rekodi wa pauni milioni 37.
No comments:
Post a Comment