KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, January 24, 2014

Kocha wa Uganda Micho atamba kupata ofa ya Botswana lakini .........

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes', Milutin ‘Micho’ Sredojevic, ametipotiwa kukataa kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Botswana.
Msebia huyo ameweka wazi kuwa alikuwa na mawasiliano na chama cha soka cha Botswana (BFA) lakini asingeweza kuiacha kazi ya kukinoa kikosi cha Uganda Cranes. 

“Ndio wamekuwa wakivutiwa na mimi na tulikuwa katika mawasiliano lakini siwezi kuipiga chini Uganda ambayo bado nina makataba,” Micho alikuwa akiongea na mtandao wa Mtnfootball.com

Micho ambaye alitimuliwa kazi na Rwanda mwezi April mwaka uliopita, baadaye aliajiriwa kuifundisha Uganda Cranes baada ya kuwashinda makocha takribani 37 waliokuwa wanafukuzia kazi hiyo.
Ameiongoza Uganda Cranes kushika nafasi ya tatu katika michuano inayoendelea ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani katika kundi B nchini Afrika kusini.

Pia aliifikisha Cranes katika robo fainali ya michuano iliyopita ya CECAFA ambayo timu ya taifa ya Kenya Harambee stars walitawazwa kuwa mabingwa wapya.

Mafanikio makubwa kuwahi kuyapata akiwa na timu ya taifa ya Rwanda maarufu kama Amavubi ilikuwa ni mwaka 2011 pale ambapo walimaliza katika nafasi ya pili katika michuano mikubwa ya 'Cecafa Senior Challenge, the East and Central African regional Championship'.

No comments:

Post a Comment