Kiungo wa timu ya taifa ya Cameroon Stephane Mbia amekuwa akisumbuliwa na majeraha ambayo yatamuweka nje ya uwanja mwezi huu hususani kuelekea katika mchezo wa hatua ya mtoano kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia dhidi ya Tunisia.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 aliumia mguu wakati akiitumikia klabu yake ya Sevilla, ambapo taarifa zanasema kuwa kiungo huyo atakuwa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mzima.
Hii ina maanisha kuwa Oktoba 13 hatakuwepo uwanjani kama ilivyo katika mchezo wa marudiano katikati ya mwezi Novemba, ambapo mshindi wa mchezo huo atakuwa akielekea katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment