Luiz Felipe Scolari amethibitishwa
kuwa meneja mpya wa timu ya taifa ya Brazil kufuatia kuondolewa mtangulizi wake
Mano Menezes wiki iliyopita.
Taarifa zilizokuwa zimezagaa
tangu jumatano zilikuwa zinaashiria Scolari
kupewa nafasi hiyo na jana shirikisho la soka la Brazil likamthibitisha kurejea
kukiongoza kikosi cha timu ya timu ya taifa ya Brazil.
Scolari aliiongoza Brazil mpaka
kunyakua taji la kombe la dunia mwaka 2002 na atakuwa kiongozi wa benchi la
ufundi la mabingwa hao mara tano wa kombe la dunia kwenye fainali za mwaka 2014
ambalo Brazil ndio wenyeji.
Bosi huyo wa zamani wa Chelsea
alikuwa nje ya kazi tangu alipoachana na Palmeiras mwezi September, ambapo
kabla ya alikuwa akikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Ureno katika fainali
za kombe la duna za mwaka 2006 na mwaka 2004 na 2008 michuano ya Ulaya.
Amenukuliwa baada ya uteuzi
wake akisema
"najisikia raha na kuwa
tayari, najihisi kijana , najihisi naweza,
tunalazimika kushinda taji, kwasasa hatuonekani kama tunauwezo huo lakini
tunapaswa kuwepo katika wale wanaotajwa kushinda taji. Kuwa katika nafasi ya
tatu au nne si kitu kizuri kwa nchi ambayo imechukuwa taji hilo mara tano.
"sijihisi kuwa kwenye
shinikizo najisikia furaha. Wakati Rais wa FA Marinaliponiita jumanne na
kuthibitisha nimechaguliwa nilimshukuru kwa zaidi ya mara elfu moja.
"nilikuwa kwenye presha
nilikuwa kwa mara ya kwanza tulipokuwa katika hatari ya kutokwenda kwenye
fainali ya kombe la dunia''.
Pep Guardiola alikuwa kwenye
orodha ya watu ambao walipewa nafasi katika kazi hiyo lakini Rais wa FA ya
Brazil Jose Maria Marin ameweka wazi kuwa sifa kuu iliyompa kazi Scolari ni
mafanikio yake katika ngazi ya kimataifa.
Atakuwa akisaidiwa na kocha
mwingine aliyewahi kushinda kombe la dunia Carlos Alberto Parreira, ambaye aliiongoza
Brazil mwaka 1994 kwenye fainali za nchini Marekani na sasa anarejea kama
meneja.
Marin amenukuliwa akisema,
"Baada ya kuchambua na kufikiria kwa muda
mrefu ni akiina nani watakuwa bora katika soka la Brazil, kwa mashabiki wa Brazil,
tuna mkabidhi jukumu la timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya ‘Confederations’
majira ya kiangazi na kombe la dunia, hivyo tuliona watu ambao walipata
mafanikio mara mbili na ambao wanaheshimika kote duniani , ni Felipe and
Parreira.''
Mchezo wa kwanza wa Scolari
akiwa kocha mpya itakuwa ni dhidi yEngland katika uwanja wa Wembley utakao
pigwa februari 6.
No comments:
Post a Comment