Pia shirikisho la soka la Senegal
(FSF) limepigwa faini ya dolari za kimarekani za US$100,000 kufuatia vurugu za
mashabiki zilizo tokea katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya
Afrika 2013 dhidi ya Ivory Coast.
Simba hao wa Teranga sasa watalazimika
kusaka uwanja mwingine katika michezo yake ya kampeni kuwania kucheza kombe la dunia
dhidi ya Angola na Uganda.
Senegal ilipoteza matumaini
na kupeteza sifa ya kufuzu baada ya mashabiki wake kuanza vurugu za kurusha
mawe na kuwasha moto uwanjani kunako dakika ya 76 wakati huo wakiwa nyuma kwa
ushindi wa jumla wa mabao 6-2.
No comments:
Post a Comment