Adel Taarabt ameitwa tena katika kikosi cha Morocco ikiwa ni miezi tisa baada ya kumaliza mgomo wake wa kumuomba radhi kocha wa kikosi hicho baada ya kumtusi.
Kiungo huyo ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Fulham akitokea QPR, yumo katika kikosi cha Morocco kitakacho cheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Afrika kusini Oktoba 11.
Mwezi Januari, Morocco ilitaka kuombwa radhi na Taarabt
kufuatia kumtusi Rachid Taoussi, ambaye baadaye aliaachwa katika kikosi kilicho shiriki michuano ya Mataifa ya Afrika.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 alishutumiwa kwa kutokuwa na nidhamu kwa kocha wake.
Kocha Taoussi alimuacha kikosini Taarabt baada ya kuonyesha dharau kufuatia kukataa kukutana naye na hata kugomea kupokea simu yake pale baada ya kuchelewa kujiunga na kikosi kwa safari ya maandalizi barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment