Wayne Rooney aliachwa na Manchester United katika mchezo wa Community Shield
Roy Hodgson kumpa nafasi Rooney
Meneja wa kikosi cha timu ya taifa ya England Roy Hodgson ameziweka kando taarifa zinazo muhusu mshambuliaji Wayne Rooney kuwa ni majeruhi wakati huu akijiwinda na machezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Scotland.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hakucheza mchezo wa ngao ya jamii (Community Shield) kufuatia kusumbuliwa na bega hizi zikiwa ni taarifa kutoka katika klabu yake ya Manchester United, lakini kwa upande wake Hodgson amesema hakuna ushahidi wa hilo zaidi.
Menukuliwa Hodgson akisema
'Ni ngumu kujua kwa macho ni kiasi gani mtu mzima alivyo lakini hakuna shaka kuwa alikuwa akuumwa majeraha.
'Tunazo data kutoka katika mazoezi yetu na itakuwa vema kujua hilo lina ukubwa gani. Kwa kuwa amekuwa na majeraha hataweza kufanya mazoezi kama tulivyofanya leo.
'Amekuwa akifanya mazoezi binafsi kwasababu Manchester United ilicheza michezo kadhaa lakini alikuwa akifanya mazoezi ya kujenga mwili na leo alikuwa katika mazoezi ya kucheza mpira.
'Nimekuwa nikiendelea kuongea naye tangu tulipoanza mazoezi lakini nategemea atakuwa vizuri.
Theo Walcott , Alex Oxlade-Chamberlain na Rickie Lambert kwa pamoja katika mazoezi ya
'Sitaki kuongelea juu ya kama hachezi katika klabu yake kwamba pia hatacheza katika kikosi cha England. Pale atakapo patikana kwa England atacheza kwasababu ni mmoja kati ya wachezaji wetu bora'.
Rickie Lambert akipasha pamoja na Jack Wilshere kushoto na Steven Gerrard
Rooney akiwa na Jermain Defoe
No comments:
Post a Comment