Shirikisho
la mchezo wa mpira wa kikapu Tanzania TBF Limeishukuru serikali kwa kuendelea
kulisapoti katika juhudi zake za kuuendeleza mchezo wa mpira wa kikapu hapa nchini , hasa
linapoandaa clinic mbalimbali.
Mbali na shukurani hizo TBF imeiomba serikali kuangalia
suala zima la miundo mbinu ya viwanja vya mchezo huo.
Kauli hiyo ya TBF imetolewa na Rais wake Musa Mziya wakati wa ufunguzi wa Clinic ambayo iliendeshwa kwa siku mbili na wacheza kikapu maarufu katika ligi ya mchezo huo nchini Marekani NBA Hashim Thabiti mtanzania na Luo Ben ambaye
ana asili Sudani wa kusini mwenye uraia wa Uingereza anayeichezea Chikago bulls.
.
Akizungumza katika hotuba ya ufunguzi wa klinic hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco na kuanzia jana na kumalizika leo , Rais wa TBF Mussa Mziya amesema pamoja na mchezo huo kuendelea kupata sapoti
ya wahisani mbalimbali lakini uhaba wa viwanja kwao ni kikwazo
Bofyahapa
Ama kwa
upende wake Naibu Mkurugenzi wa michezo Tanzania Juliana Yasoda amesema serikali
ipo bega kwa ubega katika kuendeleza michezo na itaendelea kufanya hivyo,kwa kuweka na kuandaa mazingira mazuri ya kuwalinda na kuwasaka wafadhili wapya
Bofya hapa
Bofya hapa
No comments:
Post a Comment