KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, August 25, 2012

KIMATAIFA:Rio Ferdinand kurejea uwanjani wiki ijayo: Alex Fergsuon,Xavi: Nataka kuendelea kuwa muhimu Barcelona,Liverpool yathibisha mkopo wa Sahin na Ricaldo Kaka kurejea AC Milan.


Rio Ferdinand kurejea uwanjani wiki ijayo: Alex Fergsuon
Mlinzi wa kati wa mashetani wekundu Rio Ferdinand huenda akarejea kikosi cha kwanza cha Manchester United wiki ijayo hii ikiwa ni kwa mujibu wa Meneja wake Sir Alex Ferguson.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 33 alikosekana katika mchezo wa ufunguzi wa msimu jumatatu dhidi ya Everton mchezo ambao United ilifungwa kwa bao 1-0.
Ferdinand anayesumbuliwa na groin anatarajiwa kuwa kuwepo kikosini katika mchezo dhidi ya Southampton.
Kiungo wa pembeni  Antonio Valencia aliziba nafasi ya ulinzi wa kulia kule Goodison Park, lakini meneja wake Sir Alex Furguson amesema Rafael atakuwa tayari amerejea wiki ijayo.
 amenukuliwa akisema
“Valencia anaweza kucheza sehemu yoyote, Yule kweli ni mmarekani ya kusini , anapenda kucheza soka ana nguvu na mwepesi na anaweza ku-tackle. ana weza kufanya mambo makubwa kucheza upande wa kulia ni kwa muda tu”.
Xavi: Nataka kuendelea kuwa muhimu Barcelona

 
 Kiungo ‘maestro’ wa Barcelona Xavi Hernandes ameweka wazi kuwa ana njaa ya kuendelea kupata mafanikio na kuendelea kuwa ni mchezaji muhimu katika klabu yake katika kampeni ya msimu wa 2012/2013 ndani ya Camp Nou.
Xavi amesema  hana mpango wa kustaafu soka la kimataifa kwasasa.
Kiungo huyo mzoefu amekuwa ni sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza misimu 15 ndani ya Catalans na anajivunia kuwa kwenye mafanikio.
amenukuliwa akisema
"nataka kufanya mambo kama hivyo msimu huu, kuendelea kuwa muhimu katika timu na kushinda mataji"
ameendelea kusema
"kiungo huyo mchezeshaji pia amezungumzia soka la kimataifa akisema kwasasa hafikirii kustaafu soka la kimataifa"
Xavi amecheza jumla ya michezo 100 ya kimataifa akiwa na La Roja, akishinda mataji mawili ya Ulaya na kombe la dunia 2010.

Liverpool yathibisha mkopo wa Sahin

 Liverpool imethibitisha kufikia makubaliano na Real Madrid kumsanisha Nuri Sahin kwa mkopo wa muda mrefu baada ya zoezi la kipimo cha afya kukamilika.
Nuri Sahin mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na Real Madrid msimu uliopita baada ya kuonesha kiwango katika klabu ya Borussia Dortmund ambayo ilitwaa taji la Bundesliga msimu wa 2010-11, na kuchukua tuzo ya mchezaji wa msimu wa ligi ya ujerumani Bundesliga.
Aidha mturuki huyo alishindwa kuonesha kuwango kizuri  katika kikosi cha kocha Jose Mourinho na kuruhusiwa kuondoka Bernabeau kwa mkopo kusaka timu atakayopata nafasi katika kikosi cha kwanza.
Vilabu kadhaa vya Premier League ikiwemo Arsenal, vilikuwa kwenye mawindo ya kupata huduma ya Sahin lakini Brendan Rodgers amefanikiwa kushinda mbio hizo.
Taarifa ya Liverpool imesema Sahin sasa atafanyiwa vipimo vya afya kule Merseyside

  Makoun ajiunga na Rennes kwa mkopo
 
 Rennes ya Ufaransa imethibisha kumpata kiungo wa Aston Villa Jean II Makoun kwa mkopo wa muda mrefu.
Mcameroon huyo alitumika msimu katika klabu ya Olympiakos ya Ugiriki kwa mkopo lakini akili yake ilikuwa kurejea nchini Ufaransa.
Meneja Pierre Dreosii amenukuliwa akisema
"tulikuwa tunatafuta kiungo mzoefu. namjua vizuri kwasababu niliwahi kumsaini nilipokuwa Lille,".
Makoun aliwasili Rennes kama mkurugenzi akichukua nafasi ya Alexander Tettey, ambaye amejiunga rasmi na Norwich ijumaa.


  Ricaldo Kaka kurejea AC Milan.
 AC Milan imeendelea kufukuzia saini ya kiungo wa Real Madrid Ricaldo Kaka na ikiwa ndio klabu yenye nafasi kubwa kunasa saini hiyo licha ya vilabu vya Uingereza Manchester United, Chelsea na Tottenham kutoa offer zao.
Mazungumzo yamekuwa yakiendelea baina ya vilabu hivyo na Real Madrid,lakini Milan inaonekana kuwa na kisu kikali zaidi kumrejesha San Siro kiungo wake wa zamani.
Taarifa zinasema mpango wa kumpelekea Kaka aidha Spurs au Chelsea kwa mkopo umetupiliwa mbali na sasa kigogo cha soka nchini Hispania Milan inaonekana kuwa kwenye mwuelekeo wa kumpata kiungo mshambuliaji huyo huku mipango ya Luka Modric ikiendelea.
Kwa kipindi kirefu mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich amekuwa akimtamani Kaka lakini mpango wa The Blues kujenga upya kikosi kwa kutumia vijana unakwamisha kusajiliwa kwa wakongwe.

  Oxlade-Chamberlain :Naweza kuziba pengo la Alex Song Arsenal


Alex Oxlade-Chamberlain anasema yuko tayari kuziba pengo la Alex Song katika klabu ya Arsenal kufuatia kuondoka kwake na kujiunga na Barcelona.
Baada ya Song kuondoka kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £15 kuelekea kwa kigogo cha Catalan na wakati huo huo kuna mazungumzo baina ya Arsenal na Real Madrid juu ya kukamilishwa kwa mkopo wa Nuri Sahin, Arsenal imesalia na kiungo dhaifu ambacho kinahitaji kuimarishwa.
Oxlade-Chamberlain mwenye umri wa miaka 19 amesema yeye anao uwezo wa kujaza sahani na kuvaa viatu vya Song.
Oxlade-Chamberlain alikuwa akitumika kama winga, lakini Arsene Wenger anaamini huenda baadaye akacheza sehemu ya kiungo ambayo alitumika katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AC Milan michuano ya vilabu bingwa msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment