Baada ya
hapo jana mabingwa wa michuano ya kombe la kagame Yanga kuanza vizuri ziara
yake nchini humo kwa kuwafunga Rayol sports mabao 2-0 ,kikosi hicho kitashuka
dimbani tena hapo kesho kwa kucheza na maafande wa polisi.
Yanga
wametua nchini Rwanda jumanne ya wiki hii ambapo alhamis walikutana na rais wa
nchi hiyo Paul Kagame katika ikulu ya Rwanda wameelekea nchini humo kwa ziara
ya wiki moja kama sehemu ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara
iliyopangwa kuanza kutimua vumbi September 15.
Akizungumza na ROCKERSPORTS moja kwa moja kutoka nchini Rwanda kocha msaidizi wa yanga Fred
Felix Minziro amesema kwamba ziara yao ya nchini Rwanda imekuwa nzuri
Bofya hapa
ARUSHA
Tukitoka nchini Rwanda tuelekee katika jiji la Arusha ambapo mabingwa wa soka Tanzania bara simba hapo kesho nao watakuwa katika mchezo wao wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki tokea walipoweka kambi jijini humo kwa kucheza na timutimu ya Mathare united kutoka nchini Kenya.

Menejea wa
simba Nico nyagawa ameongea na ROCKERSPORTS toka jijini Arusha kuwa wanaamicni mchezo huo wa kesho
utatumika kama sehemu ya mwalimu wao Milovan Circovic kukiangalia kikosi chake
kama kipo vizuri kabla ya kuwakabili Azam united katika mchezo wa ngao ya Jamii
mapema mwezi ujao.
Bofya hapa
No comments:
Post a Comment