Yanga-Mbiwa:Siwezi kusema no kuelekea
AC Milan.
Nahodha wa Montpellier
Mapou Yanga-Mbiwa ameweka wazi kuwa huenda akafikiria juu ya kuelekea AC Milan.
Nahodha huyo
mwenye umri wa miaka 23 alikuwa akihusishwa na kutaka kuelekea kwa mabingwa hao
mara saba wa ulaya msimu huu wa uhamisho wa kiangazi baada ya kampeni ya msimu
wa 2011-12 maarufu kama ‘La Mosson’ ambapo aliiongoza timu yake kutwaa taji la Ligue
1.
Yanga-Mbiwa amesisitiza
kuwa licha ya kuendelea kuwepo katika klabu hiyo lakini hakuna mazungumzo
yaliyofanyika juu yangu msimu huu wa uhamisho na kwamba ataendelea kusalia
kwenye kampeni ya sasa.
Mlinzi huyo
wa kati mzaliwa wa Bangui amenukuliwa na Telefoot akisema,
"huwezi
kusema hapana kuelekea Milan. mpaka sasa hakuna makubaliano ingawa bado nipo Montpellier,"
"Lakini hatujui nini kimetokea katika
siku za mwisho za kipindi cha uhamisho. tutaliandalia hilo. katika maisha
unatakiwa kujiamini mwenyewe.
"Kama
uhamisho hautafanikiwa mwaka, basi utafanyika mwakani."
Drogba: Nimejiunga Shanghai Shenhua kwasababu za kisoka si
na pesa
Didier
Drogba amesisitiza kuwa pesa si kitu kilicho pelekea kuamua kujiunga na Shanghai
Shenhua ya Uchina baada ya kuondoka Chelsea.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Tembo wa Ivory alihamia mashariki mwezi June baada ya
utumishi wake wa miaka minane Stamford Bridge na kusema kuwa mpango wake wa
kuelekea huko ulikuwa wa kisoka zaidi.
Drogba anaamini
bado ana mengi ya kutoa kama mchezaji akiwa China na kuongezea kuwa pengine
asingepata changamoto ya kutosha endapo angeendelea kusalia Ulaya.
Amenukuliwa
na Telefoot akisema
" Hii
si kama dhahabu, ni maamuzi ya kisoka . Naamini ni sawa . Na ninaamini nimeleta
kitu kipya katika klabu yangu.
Amewakosoa
wanaosema kuwa amekwenda kumalizia soka yake kabla ya kustaafu akisema hiyo ni sehemu
ya maisha yake ya soka.
Mshambuliaji
wa zamani wa Uingereza Michael Owen, ambaye ameachwa na Manchester United msimu
huu anaamini atapata klabu nyingine ya kuitumikia kabla ya kufungwa kwa kipindi
cha usajili.
Owen mwenye
umri wa miaka 32,aliachwa na United baada ya misimu mitatu ndani ya Old Trafford lakini mshambuliaji huyo wa
zamani wa Liverpool, Real Madrid na Newcastle anasema ana matumaini anaweza
kupata nafasi katika moja ya timu za ligi kuu ya nchini Uingereza Premier
League.
Amenukuliwa na
BBC Radio akisema,
"katika
hali ya aina hii kuna mengi ambayo yanaweza kutokea baadaye kwa kuwa watu bado
wanaviangalia vikosi vyao na mambo kama hayo.
"Kwa
hiyo, ndiyo nimekuwa na mawasiliano na vilabu vichache lakini naamini nitapata
jezi nyingine hivi karibuni "
Rooney 'nje wiki nne'
Mshambuliaji
wa Manchester United Wayne Rooney anakabiliwa na uwezekano wa kuwa nje ya
uwanja kwa wiki nne baada ya kupata mchubuko mkubwa paja katika mchezo wa jana
dhidi ya Fulham ambao United ilishinda kwa mabao 3-2.
Inavyoonekana
mshambuliaji huyo huenda akakosa michezo kadhaa ya klabu yake na kimataifa
wakati huu ambapo England ikiwa na michezo miwili ya kimataifa dhidi ya Macedonia
na Ukraine mapema mwezi September, lakini pia klabu yake United ikitaraji
kucheza dhidi ya Southampton, Wigan na Liverpool mwezi ujao.
Rooney
alitolewa uwanjani zikiwa zimesalia dakika 20 alikumbana na dhoruba hiyo wakati
akikabiliana na Hugo Rodallega na kulazimika kubebwa kwenye machela wakati
akijaribu kuzuia mpira ndipo ‘njumu’ za mshambuliaji wa Fulham zikamparua
pajani.
Meneja wake Sir
Alex Ferguson amethibitisha baada ya mchezo kuwa Rooney atahitaji kupata
matibabu ambayo yatamuweka nje ya uwanja katika kipindi cha mwezi mmoja.
Akiongea na
Sky Sports amesema,
"Ni
mchubuko mbaya . amepelekwa Hospitali na atakuwa nje ya uwanja baada ya wiki
nne,"
Katika
mchezo huo , Fulham ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tatu kupitia
kwa Damien Duff.
United ikajibu
kwa mabao matatu ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Robin van Persie, Shinji
Kagawa na Rafael.
Kujikanganya
kwa David de Gea na Nemanja Vidic kulipelekea mlinzi wa kati Vidik kujifunga na
kuandika bao la pili kwa Fulham zikiwa zimesalia dakika 25 kabla ya mchezo huo
kumalizika.
Rais wa Santos anasema Ganso lazima
akubali kuzomewa na mashabiki
Rais wa
klabu ya Santos ya nchini Brazil Luis Alvaro de Oliveira Ribeiro amesema ni
lazima nyota wa kimataifa wa Brazil Ganso akubali kuzomewa na mashabiki wa
Santos kufuatia kauli yake kuwa angependelea kuvaa jezi ya Sao Paulo, ambao ni
wapinzani wao wakubwa katika soka la Brazil wenye maskani yao pande za Peixe.
Katika
mchezo ambao Santos walishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Palmeiras usiku wa jana mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa akizomewa muda ikiwa ni hasira za
mashabiki kujibu kauli yake.
Rais wa
klabu hiyo Luis Alvaro de Oliveira Ribeiro amesisitiza kuwa ndio watu wa kwanza
na hiyo ndiyo ilikuwa salamu zao kwa Ganso na anapaswa kukubali hilo.
Ribeiro
amenukuliwa na Lancenet akisema
"Mashabiki
lazima waheshimiwe . kama msanii anapanda jukwaani lazima akubali kuzomewa au
kushangiliwa. Na katika soka ni hivyo hivyo, hiyo ndiyo kawaida" .
"Mshabiki walifuata na walikuwa na kasira
kufuatia kauli ya mchezaji huyu."
Ganso mwenyewe
amejibu kauli ya Rais wake Ribeiro akisema Rais wake hakupaswa kutoa maneno
hayo lakini amesisitiza kuwa ataendelea kutoa huduma katika klabu hiyo.
Serikali ya Malawi
imeufunga uwanja wa taifa wa nchi hiyo ulioko Blantyre miundo mbinu ya uwanja
huyo kuwa mibovu pamoja na hofu ya usalama.
Waziri wa
michezo wa Malawi Enock Chihana ana
matumaini kuwa Kamuzu stadium utakuwa tayari kutumika kwa ajili ya mchezo wa
pili wa marudiano kati ya Malawi dhidi ya Ghana kuwania kufuzu fainali za mataifa
ya Afrika 2013 mchezo ambao umepangwa kufanyika October 14.
Amenukuliwa
Chihana akisema
"tuna
matumaini kuwa mambo ya msingi ikiwa na ukarabati pamoja na vifaa muhimu vya kiusalama
yatakamilishwa ndani ya wakati kabla ya mchezo huo"
Amesema Kinga
ni bora kuliko tiba na hi hivyo serikali tumeliona hili kwa mustakabi wa watu
wetu na si vizuri kupeleka michezo yetu katika uwanja huru kama Zambia.
Serikali kwa
kushirikiana na chama cha soka cha Malawi (Fam) wamesema wana matumaimni ya kumaliza
tatizo hilo haraka iwezekanavyo.
Naye Rais wa
Fam, Walter Nyamirandu ameeleza juu ya kufungwa kwa uwanja huo akisema ni pigo
lakini ni hatua muhimu kwa faida ya mashabiki wa soka na Malawi yenye kama
nchi.
Kufungwa kwa
uwanja huo kumekuja wakati ambapo kunatarajiwa kufanyika kwa fainali ya Presidential
Cup kati ya Big Bullets na Moyale Barracks ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika
hii leo na sasa mchezo huo umepangwa kufanyika September 1.
Fainali hiyo
imehamishiwa Civo Stadium ulioko katika mji mkuu wa Malawi, Lilongwe.
Fifa imekuwa
ikitoa tahadhari kwa Malawi kupunguza uwezo wa watazamaji katika uwanja huo
kutoka 60,000 mpaka 32,000.
No comments:
Post a Comment