Mada Maugo |
Mwanamasumbwi machachari Mada Maugo amesema hana mpango wa kucheza tena ngumi na mabondia wa Tanzania hata
akipewa ahadi ya pesa nyingi.
Mada ametoa
kauli hiyo alipokuwa akiongea na Rockersports akisema sababu kubwa ni ngumi za
Tanzania kutawaliwa na mambo ya ushirikina ambayo yamekuwa yakionyeshwa na
hadharani huku wadau na viongozi wakikosa njia ya kumaliza aibu hiyo.
Kwasasa anajipanga kuelekea nchini Marekani mwezi Novemba ambapo atakuwa na pambano na bondia wa huko ambaye hata hivyo hakuwa tayari kumtaja jina lake mpaka atakapo pata idhini ya mtayarishaji wa pambano hilo ambaye ni mmarekani.
Kwasasa anajipanga kuelekea nchini Marekani mwezi Novemba ambapo atakuwa na pambano na bondia wa huko ambaye hata hivyo hakuwa tayari kumtaja jina lake mpaka atakapo pata idhini ya mtayarishaji wa pambano hilo ambaye ni mmarekani.
Mada
ametolea mfano hivi karibuni kujitokeza mambo kama hayo ambapo bondia mmoja
alikwenda kupiga kambi nchini Msumbiji na kurejea nyumbani Tanzania akiwa na
lundo la waganga wa kienyeji.
Amesema
kwasasa malengo yake ni kucheza na mabondia wa nje na amejikita zaidi na
kuangalia mapambano ya nje.
Mada Maugo amesema
wakati jitihada za kupigana na matumizi ya bangi kwa mabondia wa Tanzania
zikiwa zinaonekana kufanikiwa changamoto ya matumizi ya nguvu za giza imekuwa
ni kubwa hivyo yeye ameona ni bora akaachana na mabondia wa nyumbani na
kuelekea katika nje ya nchi.
Ametolea mfano pambano la Francis Cheka na Japhet Kaseba la hivi karibuni uwanja wa Taifa ambalo hata hivyo halikufanyika, akisema pambano hilo liligubikwa na mambo ya kishirikia ambapo inesemekana Cheka alikuwa nchini Msumbiji kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo wakati ambapo Kaseba alikuwa mkoni Kigoma ambaye alikuja katika pambano hilo akiwa na mashekh tayari kumdhoofisha mpinzani wake.
BOFYA HAPA KUSIKILIZA
Japhet Kaseba |
Fransis Cheka |
No comments:
Post a Comment