Paulo Bento atasalia kuwa kocha wa Ureno mpaka mwishoni mwa michuano ya Euro 2016 baada ya kukubali kuongeza mkataba wa miaka miwili.
Bento mwenye umri wa miaka 44 raia wa Ureno aliaajiriwa mwaka 2010 ambapo mkataba wake wa sasa ulitarajiwa kumalizika Julai mwaka huu.
Bento ameiongoza Ureno mpaka kufikia nusu fainali ya Euro 2012, kabla ya kupoteza kwa waliokuwa mabingwa Hispania na pia wakiwaongoza mpaka kiangazi kwenye kombe la dunia.
Ureno itakutana na Ujerumani, Marekan na Ghana katika kundi G katika fainali ya kombe la dunia nchini Brazil.
Kiungo Bento aliwahi kuichezea Ureno jumla ya michezo 35 katika uchezaji wake katika timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment